Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA KAGERA, MAMA MWENYE MTOTO WA MIEZI MINNE PAMOJA NA MUMEWE WAUAWA KINYAMA

 

 Mwili wa mwanaume ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa kwa kukatwa Mapanga na watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi.
Mwili wa mwanamke ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa na majambazi hao. 
 Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia na kuwaua mume na mke na kumjeruhi mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyeachwa na mama yake aliyeuawa katika tukio lililotokea kijiji cha Murvyagira wilayani Ngara mkoani Kagera Ijumaa ya Agost 08,2014.

Kwa mujibu wa mtoto mkubwa wa marehemu amesema majambazi hao walivamia nyumbani kwao majira ya saa 3 usiku ambapo walitumia panga na jembe kuwaua baba na mama yake na kisha kuwapora Maharage gunia moja, Radio, Gunia la Karanga, Mabati na Fedha vitu ambavyo hadi sasa thamani yake haijajulikana, huku wahalifu hao wakitokomea kusikojulikana.
Aidha baadhi ya wananchi walioongea na mwandishi wetu, wameomba juhudi ya kuimarishwa hali ya usalama na ulinzi wilayani Ngara izidishwe hasa wakati huu ambako matukio ya mauaji yamezidi kujitokeza.
Mama huyo ameacha Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyejeruhiwa na watu hao wanaodhaniwa ni majambazi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top