Mwandishi wa habari, Ephraim Kibonde jana aliachiwa kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam alikokuwa akishikiliwa tangu mwishoni mwa wiki kwa tuhuma za kusababisha ajali ya gari na kutoa lugha ya matusi kwa askari wa usalama barabarani.
Mwanahabari huyo alikamatwa Jumamosi asubuhi kwa tuhuma za kusababisha ajali hiyo na kuendsha gari akiwa amelewa.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius
Wambura alithibitisha jana kukamatwa kwa Kibonde na kwamba walikuwa
wakiendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
“Tangu juzi asubuhi alikuwa bado anashikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa,” alisema Kamanda Wambura.
Hata hivyo taarifa zilizopatikana jana jioni zilidai kuwa Kidonde aliachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi ukiendelea.
Hata hivyo taarifa zilizopatikana jana jioni zilidai kuwa Kidonde aliachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi ukiendelea.
Kwa upande wake, mkuu wa Kituo cha Polisi cha
Oysterbay, Victor Samata alikataa kuzungumzia tukio la kukamatwa Kibonde
kwa madai kuwa si msemaji.
“Siwezi kuzungumza lolote kwa sasa. Zipo mamlaka zinazohusika na vyombo vya habari,” alisema Samata.
Kibonde anadaiwa kuendesha gari akiwa amelewa, hali iliyomfanya kugonga gari nyingine kwa nyuma.
Inadaiwa pia kuwa, baada ya kusababisha ajali hiyo
akiwa na mwandishi mwenzake, Gadner Habash, walikimbia wakati polisi
wakitaka kupima eneo la ajali.
Baada ya kukimbia, polisi walimfukuza kwa kutumia gari jingine kabla ya kumkamata eneo la Ubungo.
Kibonde na mwenzake baadaye walipelekwa eneo lililotokea ajali kwa ajili ya kupima na baadaye kupelekwa kituo cha polisi.
Post a Comment