Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mamunyange Azinduwa Uwanja wa Michezo ya Majeshi Zanzibar.


Waandishi wakipata maelekezo ya Uzinduzi wa Uwanja Mpya wa Michezo ya Majeshi Zanzibar katika kambi ya migombani ulifunguliwa na Mkuu wa Majeshi Tanzani Jenerali Davis Mamunyange.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, akikata utepe kuashiria kuufunguauwanja mpya wa michezo ya majeshi Zanzibar yanayotarajiwa kufunguliwa kesho na Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, katika uwanja wa Amaan, jumla ya nchi tano zinashiriki michezo hiyo Tanzania, Kenya, Uganda Ruwanda na Burundi.kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi Mhe.Abdallah Mwinyi Khamis na kulia Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Shariff Shekh  Othman.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Davis Mwamunyange, akiwa na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Shariff Shekh Othman kulia na kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mjini wakimshindikiza Mkuu wa Majeshi kukagua timu baada ya ufunguzi wa uwanja huo wa michezo ya Majeshi Migombani Zanzibar.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamungyange, akiikagua timu ya Vikosi vya SMZ, baada ya Kuuzindua Uwanja Mpya wa Michezo ya Majeshi, yanayotarajiwa kufunguliwa kesho uwanja wa Amaan na Rais wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamungyange, akiikagua timu ya JWTZ, baada ya Kuuzindua Uwanja Mpya wa Michezo ya Majeshi, yanayotarajiwa kufunguliwa kesho uwanja wa Amaan na Rais wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, 
Kikosi cha timu ya Vikosi vya SMZ kinachishiriki michuano ya Tamasha la Michezo ya Majeshi wakiwa katika mazoezi kabla ya mchezo wa kirafiki na timu ya Vikosi vya SMZ, wakati wa uzinduzi wa Uwanja mpya wa Michezo ya Majeshi Zanzibar.inayotarajiwa kufunguliwa kesho uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Jeshi laWananchi Tanzania kinachishiriki michuano ya Tamasha la Michezo ya Majeshi wakiwa katika mazoezi kabla ya mchezo wa kirafiki na timu ya Vikosi vya SMZ, wakati wa uzinduzi wa Uwanja mpya wa Michezo ya Majeshi Zanzibar.inayotarajiwa kufunguliwa kesho uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mamwunyange, akifuatilia mchezo wa kirafii kati ya JWTZ na Timu ya Vikosi vya SMZ, timu hizo zinashiriki michezo hiyo inayotarajiwa kufunguliwa kesho uwanja wa Amaan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein. 
                                                                   hupiti wala kutowa pasi
Kizazaa golini mwa timu ya JWTZ wakati wa mchezo wa kirafiki kuzinduwa uwanja mpya wa michezo ya majeshi uliofunguliwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, ikiwa ni maandalizi ya michezo ya 8 ya Majeshi mwaka huu yanafanyika Zanzibar yanayotarajiwa kufunguliwa kesho uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mchezaji wa timu ya Vikosi vya SMZ akijiandaa kutowa pasi wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika katika sherehe za Ufunguzi uwanja mpya  utakaofanyika michezo ya 8 ya Majeshi Zanzibar. 
Mchezaji wa timu ya JWTZ mwenye mpira akijiribu kutowa pasi na huku mchezaji wa timu ya Vikosi vya SMZ akijirabi kumzuiyawakati wa mchezo wa kirafii wa uzinduzin wa uwanja huo migombani bavuai.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mamunyange akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya sherehe ya Ufunguzi wa Uwanja mpya wa michezo ya Majeshi Zanzibar ukiwa na uwezo wa kuchezwa michezo Minne kwa wakati tafauti, Mchezo wa Mpira wa Kikapu, Mchezo wa Netiball, Mchezo wa Mpira wa mikono, uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya michezo Migombani.  
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top