Kijana huyo ambaye jina halijafahamika akiwa amefariki baada ya Kuchomwa kisu na mwenzake kisa madai ya Tsh 5000 tuu
Mwili wa mpiga debe huyo baada ya kifo chake |
DENI
la Sh 2,000 limetosha kumaliza uhai wa mpiga debe maarufu wa stendi ya
mabasi yaendeayo mikoani ya mjini Iringa, Samwel Yengayenga baada ya
kuchomwa kisu mara mbili katika eneo la mgongoni na kifuani.
Tukio
hilo la kinyama limetokea leo majira ya saa 6.55 mchana baada ya
Yengayenga na mtuhumiwa wa mauaji yake aliyekuwa akidai kiasi hicho cha
fedha kurushiana maneno makali na kisha kupigana.Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani
Mungi alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Festo Ruben Mkalala (26), muosha
magari, mkazi wa mjini Iringa ambaye alikamatwa mara baada ya kufanya
tukio hilo.
Mungi
alisema Yengayenga, Mkalala na mtu mwingine wa tatu (hakumtaja jina)
wanadaiwa siku nne zilizopita waliosha basi la Kimotco linalofanya
safari zake kati ya Iringa na Arusha.
“Stahiki ya kazi hiyo ilikuwa Sh 15,000; hata hivyo hawakulipwa fedha hizo baada ya kumaliza kazi hiyo,” alisema.
Alisema
siku iliyofuata Mkalala na kijana huyo mwingine waliyefanya naye kazi
walikwenda kuchukua ujira wao na kugawana Sh 5,000 kila mmoja huku
Mkalala akiahidi kutunza Sh 5,000 za Yengayenga mpaka watakapokutana.
Walipokuta,
RPC alisema Mkalala alimpa Yengayenga Sh 3,000 badala ya Sh 5,000 na
kuahidi kummalizia kiasi kilichobaki kesho yake.
Kitendo
hicho kwa mujibu wa mashuhuda kinadaiwa kumchukiza Yengayenga aliyeamua
kunyanganya simu ya Mkalala mpaka amaliziwe Sh2,000 zake zilizobaki.
Kamanda Mungi alisema Mkalala alichukizwa na uamuzi huo na kuanzisha ugomvi uliopeleka kifo cha Yengayenga.
“Uchunguzi
wa awali unaonesha Mkalala aliamua kupigana na Yengayenga ili
arudishiwe simu yake na alipozidiwa alikimbia kusikojulikana na kurudi
akiwa na kisu mkononi,” alisema.
Ili
kuipata simu yake, Kamanda Mungi alisema ushahidi wa awali unaonesha
Mkalala alitumia kisu hicho kumchoma mgongoni na kifuani Yengayenga na
kusababisha mauti yake.
Yengayenga
alikufa papo hapo katika tukio ambalo mtuhumiwa huyo alikamatwa na
kufikishwa kituo cha Polisi cha kati cha mjini Iringa.
Post a Comment