NDUGU wawili wameuawa na majambazi
waliovamia baa eneo la Mwananyamala kwa Mama Zacharia, jijini Dar es
Salaam na kupora mkoba uliokuwa na fedha zaidi ya Sh milioni mbili.
Tukio hilo ni la juzi usiku na waliouawa
ni Jeremiah Tarimo (37), mkazi wa Kimara na Nestor Tarimo (49) maarufu
kwa jina la ‘Mangi Shasha’, mkazi wa Mwananyamala Kisiwani.
Hali ya taharuki ilizuka eneo hilo baada
ya wakazi wake kusikia milio ya risasi na kusababisha maduka na nyumba
kufungwa kwa hofu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,
Camillius Wambura alithibitisha tukio hilo jana na kusema lilitokea saa
1.45 usiku katika baa ya Mahamo.
Alisema majambazi hao baada ya kufanya
mauaji walitokomea na pikipiki ambayo hakuitaja namba zake za usajili
kwa sababu za kichunguzi.
Ndugu wa marehemu ambaye alikuwa na
mkoba ulioporwa, Mwajuma Jeza, mkazi wa Mbezi Louis, alisema alikuwa
amekaa kwenye baa hiyo na ndugu zake wakati wa tukio hilo.
"Mwanamke huyo alikuwa na mkoba ambao
ulikuwa na fedha karibu Sh milioni mbili, simu ya mkononi, kadi za benki
na funguo. Aliingia kijana katika baa hiyo akaenda kupora mkoba huo,
kukawa na purukushani ndipo wenzie wawili waliinuka kumsaidia," alisema
Wambura.
Wambura alisema walitokea vijana wengine
wawili ambao walivyatua risasi tatu ikampiga Jeremiah ubavu wa kulia na
kumpiga tumboni Nestor.
Alisema wale majambazi walitokomea kwa
katumia pikipiki na ndugu hao wawili walifariki wakati wakipatiwa
matibabu hospitali ya Mwananyamala.
Post a Comment