Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wema Sepetu: Najuta Kumrudia Diamond



Takribani wiki sasa kumekuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu hayuko sawa katika mahusiano yake ya kimapenzi na nguli wa Bongo Fleva, Diamond Plutnumz....

Kutokana ta taarifa hizo, Mpekuzi iliamua kupekua undani wake na ndipo ilipokutana na kilio kipya cha Wema Sepetu kuhusiana na kuzushiwa taarifa mbalimbali asizozielewa chanzo chake....

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu na Wema, imefika mahali Wema anajuta kuwa na Diamond kwa sababu ya kuandikwa kwa mambo mengi yasiyo na ukweli na yanayomfedhehesha moyoni....

Rafiki huyo amedai kuwa mara kwa mara Wema amekuwa akijiuliza sababu ya kuandikwa taarifa mbalimbali zisizo na kichwa wala miguu ambapo mwisho wa yote hupata jibu ni kwa sababu ya kuwa na mahusiano na Diamond....

"Wakati mwingine anasema angelijua bora angebaki bachela kwani kuna kikundi cha watu hakipendi kumuona akiwa na Diamond hivyo kinafanya kazi ya kumzushia taarifa zisizoeleweka kila mara kwa lengo la kumshushia hadhi," kimesema chanzo hicho.

Mwandishi alipokiuliza chanzo hicho ni kwa kiasi gani Wema anamwamini Diamond kilisema:

"Ukweli ni kwamba Wema anampenda sana Diamond lakini hamwamini kwa sababu wakati mwingine taarifa zinazoandikwa magazeti hutolewa na Diamond mwenyewe, hali hiyo inampa wakati mgumu sana Wema kujua ashike wapi na wapi apaache,"

"Unajua Diamond haaminiki, unaweza kukuta Wema anagombana na watu kumbe mtoa taarifa ni Diamond mwenyewe."
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top