Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Camilius Wambura.
Majambazi wamempora mteja Sh. milioni 19 wakati akipeleka fedha hizo
katika Tawi la Benki ya Ecobank lililoko eneo la Mwenge, jijini Dar es
Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema tukio
hilo lilitokea majira ya 11:15 jioni juzi wakati mfanyakazi wa wakala wa
fedha, Sham Msuya, ambaye ni mkazi wa Kijitonyama, akipeleka kiasi
hicho fedha katika benki hiyo.
Alisema baada ya tukio hilo, polisi walifika eneo hilo na kufanikiwa
kuokota maganda mawili ya risasi zilizofyatuliwa na majambazi hao.
“Tumepata taarifa ya tukio hilo, mfanyakazi aliyeporwa fedha jina lake
tunalihifadhi.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa, aliyeporwa tunamshikilia kwa uchunguzi zaidi,” alisema Kamanda Wambura.
Kaimu Meneja Mkuu wa Tawi hilo, Boniface Kisetu, alisema mtu aliyefanya
tukio alikuwa mmoja na alitumia usafiri wa pikipiki na bastola
kufanikisha uhalifu huo.
Shuhuda wa tukio hilo, ambaye ni mlinzi wa Kampuni ya Ultimate Security,
Mpanduli Deogratius, alisema alinusurika kifo wakati jambazi hilo
lilipofyatua risasi, ambayo alisema iliyomkosa na kugonga nguzo nje ya
benki hiyo.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment