Stori: Shakoor Jongo
PREZIDAA wa
Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Mbwana ‘Chaz Baba’ anadaiwa
nusura amtoe roho mkewe wa ndoa, Rehema Sospeter Marwa baada ya kumpiga
na kitu kizito kichwani mpaka kushonwa nyuzi ishirini.
MANENO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo karibu na wanafamilia
hao (jina limehifadhiwa), usiku wa Alhamisi iliyopita, kikiwa maeneo ya
Kinondoni jijini Dar kilishuhudia ugomvi huo baada ya kwenda kuangalia
nani anamshushia kipondo mwenzake.
Chanzo kilisema baada ya kufika, ndipo kiligundua kuwa, mwanamuziki huyo ndiye aliyekuwa akimpa kipondo mke wake.
“Dah!
Kiukweli kile si kipigo cha kumpiga mke, hasira bwana ni kitu cha ajabu
sana. Chaz anatakiwa kujiangalia sana,” kilidai chanzo hicho.MKE AFUNGUKA ‘EI TU ZEDI’
Baada ya
taarifa hiyo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta mwanamke huyo ili aeleze
nini kilitokea hadi mumewe kutaka kumkatishia maisha.“Nakumbuka siku ya
tukio nilikuwa supermarket maeneo ya Mwananyamala A (jijini Dar)
nikinunua unga wa ulezi wa mtoto, ghafla Chaz alitokea, akaniamuru
niingie kwenye gari alilokuwemo, tukaondoka kuelekea nyumbani.
“Tulipofika
maeneo ya Kinondoni, pale Meridian ndipo niliposhtukia naanza kupigwa.
Nakumbuka nilipigwa hadi nikaishiwa nguvu mpaka akatokea rafiki wa Chaz,
Hassan Kisanora na kuniokoa, nikakimbilia nyumbani,” alisema mwanamke
huyo.
CHAZ ATOWEKA, ARUDI NA SAMAKI MKUBWA
Akiendelea kuzungumza, mke huyo alisema: “Siku hiyo Chaz aliondoka na
hakurudi nyumbani mpaka alfajiri. Aliporudi aliniambia amekuja na
samaki mkubwa, yuko kwenye friji huku akisahau kuwa amenikosea na
anatakiwa kuniomba msamaha.
“Sikumjibu,
ndipo alipochukua kitu kizito na kunipiga nacho kichwani, baada ya hapo
damu nyingi zikaanza kunitoka hadi puani, niliishiwa nguvu na kupoteza
fahamu.”
“Nilipokuja kuzinduka nilikuwa hospitali kwa Dk. Mvungi, Kinondoni.
Licha ya kwamba nampenda sana lakini alitaka kuniua, hata sijui kisa.”
MADAI YA KUSHANGAZA; NDANI YA MIEZI TISA KICHAPO MARA 16
Katika kuweka mambo zaidi hadharani, mwanamke huyo aliyebahatika
kupata mtoto mmoja na mumewe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa,
tangu afunge ndoa na Chaz miezi tisa iliyopita, ameshachezea kichapo
mara kumi na sita hivyo amechoka kufanywa ngoma.“Nimechoka kufanywa
ngoma na Chaz, ndoa ina miezi tisa tu nishapigwa mara kumi na sita kati
ya hizo nimezimia mara saba kama vipi bora afanye utaratibu anirudishe
kwetu,” alimalizia kusema.
CHAZ BABA, IJUMAA WIKIENDA
Baada ya kupata maelezo ya mke, Ijumaa Wikienda lilimsaka kwa njia ya
simu Chaz mwenyewe ili azungumzie ishu hiyo ya mkewe kudai alimpiga
ambapo alipopatikana alifunguka hivi:
“Ni wivu tu kaka! Unajua mke wangu ana wivu mkali sana, alianza
kunipiga yeye mimi ndiyo nikamrudishia, hakukuwa na sababu nyingine
yoyote zaidi ya wivu,” alisema Chaz bila kufafanua.
SERIKALI YALAZIMISHA WATU KUFANYA MAZOEZI.
Serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra)
imewalazimisha watu kufanya mazoezi ya lazima baada ya kufunga kituo cha
daladala cha Mwenge jijini Dar.
Gazeti hili limekuwa
likishuhudia umati wa watu asubuhi kati ya saa 1:00 na 2:00 wakitembea
kutoka Makumbusho hadi Mwenge, hali iliyotafsiriwa kuwa serikali
imewalazimisha kufanya mazoezi bila hiyari yao.
Wakizungumzia hilo, baadhi ya raia wanaofanya kazi maeneo ya Mwenge
na Mikocheni eneo la viwanda, wamesema baada ya kufungwa kwa kituo
hicho, wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu asubuhi hivyo
kuwafanya wanapofika maeneo yao ya kazi wawe wametoka jasho sana.
“Unajua
asilimia kubwa ya tuliokuwa tunashuka Mwenge ni wa kipato cha chini,
sasa baada ya kuhamishiwa Makumbusho, tunalazimika kutembea hadi Mwenge.
“Tunachukulia kama ni mazoezi kwani baadhi tangu kuhamishwa kwa kituo
hicho sasa hivi vitambi vimepungua kwa kutembea bila kupenda,” alisema
Salum Juma wa Mbagala.
Naye John
Katuvi alisema: “Huku ni kulazimishwa kufanya mazoezi, mimi nadhani
serikali ifikirie upya uamuzi wa kuondoa kituo kile pale.“Ujue siyo wote
tunaweza kushuka Makumbusho na kuchukua tena usafiri mwingine, ndiyo
maana asubuhi utaona umati wa watu ukitembea, ukiwaona utadhani
wanafanya mazoezi kwa kupenda kumbe hawana nauli ya kuunganisha magari.”






Post a Comment