AKUNA LUGHA NYINGINE YA KUSEMA ZAIDI YA KUAINISHA KUWA PEPO WA AJALI ZA BARABARANI ZINAZOUA MAMIA YA WATU NI UZEMBE WA KUTISHA UNAOFANYWA NA MADEREVA KATIKA UENDESHAJI MAGARI BILA UTII WA SHERIA.
Uchunguzi
wa Gazeti la Ijumaa uliofanywa hivi karibuni katika maeneo mbalimbali
nchini umebaini kuwa, mbali na mwendo kasi unaotajwa mara kwa mara kuwa
unachangia ajali, suala la kutozingatia sheria za usalama barabarani ni
hatari zaidi.
Picha za
magari ya abiria yaendayo mikoani zilizotumika ukurasa wa nyuma wa
gazeti hili ni kielelezo tosha kuwa madereva wengi hawajui sheria za
usalama barabarani au wanazivunja makusudi jambo ambalo husababisha
kutokea kwa ajali nyingi za magari kugongana uso kwa uso.
Katika
ajali kubwa na mbaya iliyotokea wiki iliyopita mjini Musoma na kuua
zaidi ya watu 40, ilitokana na mabasi mawili ya J4 na Mwanza Coach
kugongana uso kwa uso katikati ya daraja; kukosa umakini kwa madereva ni
chanzo.
Uamuzi wa
kizembe kama huo na ule unaonekana katika picha zilizobeba habari hii
ambapo madereva wa magari husika wanaonekana ‘kuovateki’ kinyume cha
muongozo wa uendeshaji.Sheria zinamkataza dereva kulipita gari jingine
kwenye mlima, mteremko mkali na mahali penye kona, lakini kwa mshangao
madereva wengi wamekuwa hawazingatii hilo.
“Ukisafiri
hasa kwenye barabara kubwa kuna alama zinazokuongoza, lazima dereva
uzifuate, lakini madereva wetu hawafanyi hivyo, inawezekana hawajui
sheria au wanapuuza kwa sababu adhabu zetu ni nyepesi tofauti na nchi
nyingine kama Rwanda,” alisema Mohammed Mpinga, Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini katika mahojiano na gazeti hili hivi karibuni.
Mbali na
ulevi baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo mkoani wamekuwa wakiendesha
kwa mashindano ya kuwahi kufika waendeko ili wasifiwe na abiria kuwa
wamewawahisha jambo ambalo mwishowe kuwahi huko huwatokea puani na
kuwasababishia ajali.Taarifa ya polisi inaonesha kwamba kwa mwaka jana
pekee kulikuwa na ajali 23,842, kati ya hizo ni za mabasi 931, zilizoua
watu 313.
Post a Comment