Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt.
Nobuhiro Endo, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es
Salaam, leo Septemba 12, 2014 akiwa ameongozana na ujumbe wake kwa ajili
ya mazungumzo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Uongozi wa Shirika la NEC Corporation la Japan,
wakiongozwa na Rais wao Dkt. Nobuhiro Endo, wakati walipofika ofisini
kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 kwa ajili ya
mazungumzo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA NEC-JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed
Gharib Bilal leo amekutana na Uongozi wa Kampuni ya NEC yenye makao
yake makuu jijini Tokyo nchini Japan. Ujumbe wa NEC-Japan umeongozwa na
Rais wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya Mawasiliano na
Teknolojia, Dkt. Nobuhiro Endo.
Ujio
wa Kampuni hii nchini Tanzania unatokana na mwaliko wa Tanzania kwa
makampuni ya Japan kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Mheshimiwa
Makamu wa Rais nchini Japan, mwezi wa Mei mwaka huu. Mheshimiwa Makamu
wa Rais alitembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo wakati za ziara hiyo.
Katika
mazungumzo na uongozi wa NEC Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza
wageni wake nia ya Tanzania kuona inatanua mawasiliano na teknolojia
nchini ili kuinua uchumi na akafafanua kuwa teknolojia yoyote kutoka NEC
inakaribishwa hapa nchini ili kusaidia Tanzania kupiga hatua.
Uongozi
wa NEC nao ulimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, NEC
inaushirikiano wa karibu na Shirika la Simu Tanzania (TTCL) na kwamba
wanatarajia kukutana na uongozi wa wizara ya Mambo ya Ndani kwa lengo la
kutazama fursa za kusaidia teknolojia katika ulinzi.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam Septemba 12, 2014
Post a Comment