Rais Jakaya Kikwete
Kumekuwa na maoni tofauti kufuatia hatua ya kusitisha mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya nchini Tanzania.
Katika
kikao cha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Viongozi wa vyama vya
siasa nchini humo wamekubaliana kuwa kura hiyo ya maoni ambayo ilikuwa
ifanyike kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 kinafanyika baada ya uchaguzi
huo
Umoja
wa wabunge wa kambi ya upinzani Tanzania UKAWA hivi karibuni walisusia
bunge la Katiba na kutoka nje kwa kile walichodai kutekelezwa kwa baadhi
ya madai ya msingi.
Akizungumza
na BBC Deusi Kibamba Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini Tanzania
anasema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kusitisha vikao vya bunge
la katiba hata kabla ya muda uliopendekezwa wa Oktobar 4 mwaka huu.
Amesema
kuwa iwapo wabunge hao wataendelea na vikao hivyo wao pamoja na baadhi
ya wananchi wanatarajia kufanya maandamano hadi mjini Dodoma na kufunga
milango ya ukumbi wa bunge.
Mchambuzi
wa masuala ya kisiasa na kijamii Robert Mkosamali anasema pamoja na
kwamba fedha nyingi zimekwisha tumika hadi sasa kinachpaswa kuangaliwa
si gharama hizo bali ni kuangalia ubora wa katiba inayotafutwa hata kama
yaweza kutafutwa kwa muda mrefu na wka gharama kubwa.
Mkosamali amesema hata nchi zilizopata Katiba zilichukua muda mrefu na gharama kubwa akitolea mfano nchi ya Kenya.
Post a Comment