Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii
Aliyekuwa
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Ephraim Mgawe amekiri
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliusaini mkataba wa
kibiashara kati ya TPA na Kampuni ya China Communications Company Ltd
(CCCCL).
Mgawe
amekiri kuusaini mkataba huo wa kibiashara leo wakati akisomewa maelezo
ya awali (PH) na Wakili wa Serikali, Pius Hilla mbele ya Hakimu
Mfawidhi wa mahakama hiyo, Isaya Arufani.
Akisomewa
maelezo ya awali yanayohusiana na shtaka la matumizi mabaya ya
madaraka Mgawe alikubali wadhifa wake huo na kwamba aliusaini mkataba
huo wa kibiashara siyo kwa ajili ya ujenzi wa ghati namba 13 na namba
14 katika Bandari ya Dar es Salaam bali ni kwa minajili ya kuiwezesha
kampuni hiyo kupata mkopo nchini mwake China.
Akiendelea
kusomewa maelezo ya awali, Mgawe alikiri kuwa kampuni tano
ziliwasilisha mialiko yao ya kutaka tenda hiyo ambazo ni kampuni ya MTBS
ya Nethelands, Scott Wilson ya Uk, Ecorys ya Germany, Mott MacDonald
Maritime Consultants ya Uk, HPS Humburg ya Ujerumani, SCEC
International PTY Limited ya Australia na CPCS Transcom ya Canada.
Mshtakiwa
huyo pia alikiri kuwa kampuni ya nchini Canada ya CPCS na kutaja
gharama yao kuwa ni dola 323 za kimarekani ndiyo iliyoshinda zabuni
lakini iliyopewa kazi ya upanuzi wa bandari ni Kampuni ya China
Communications Company Ltd ya China ambayo ilitaja gharama zake kuwa ni
dola 523,131,015.97.
Hata
hivyo mshtakiwa huyo alikana kuwa baada ya kupewa taarifa hiyo ya
gharama za mradi na kampuni ya China ya CCCL alikaa kimya bila ya kutoa
kwenye bodi ya wakurugenzi.
Mgawe
na mwenzake Hamad Mussa Koshuma ambaye alikana kuwa na cheo cha Naibu
Mkurugenzi Mkuu mahakamani hapo na kudai kuwa yeye ni Mkurugenzi Mkuu
Msaidizi kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa hayo Desemba 5, 2011.
Ilidaiwa
kuwa washtakiwa hao wakati wakiwa kwenye Mamlaka ya Bandari Tanzania,
jijini Dar es Salaam, wakati wakitekeleza majukumu yao ya utumishi wa
mamlaka hiyo kwa nafasi ya mkurugenzi mkuu na naibu wake walitumia
vibaya madaraka ya kuingia mkataba wa kibiashara kati ya TPA na Kampuni
ya China Communications Company Ltd, kwa ajili ya ujenzi wa ghati namba
13 na namba 14 katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa
pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kuingia mkataba na kampuni hiyo bila
kutangaza zabuni hiyo, kinyume cha masharti ya kifungu cha 31 cha Sheria
ya Ununuzi wa Umma, namba 21 ya mwaka 2004, kwa lengo la kuinufaisha
kampuni hiyo.
1 comments:
next time muandike taarifa zenye uhakika sio kutunga maneno
ReplyPost a Comment