Dennis Kimetto.
MWANARIADHA
raia wa Kenya, Dennis Kimetto leo amevunja rekodi ya mbio za marathon
jijini Berlin nchini Ujerumani kwa ushindi wake wa saa 2, dakika 2 na
sekunde 57.
Kijana
huyo mwenye umri wa miaka 30, amevunja rekodi hiyo akipunguza sekunde
26 katika rekodi iliyowekwa na Mkenya mwenzake Wilson Kipsang ya 2: 03:
23 katika mashindano hayo yaliyofanyika mwaka jana jijini Berlin.
Kimetto
amesema: "najisikia vizuri maana nimeshinda mashindano magumu, nilikuwa
fiti tangu mwanzo wa mbio hizo na wakati nikikaribia kumaliza nilihisi
kuwa nitashinda na kuvunja rekodi"
on Tuesday, September 30, 2014
Post a Comment