Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS KIKWETE KUZINDUA BARABARA YA MWENGE –TEGETA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge –Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9 katika eneo la Lugalo, jijini Dar es salaam.  

Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar esalaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Muhandisi  Musa Iyombe imeeleza kuwa sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo zitafanyika tarehe 1, Oktoba ,2014 katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe kuanzia saa nne asubuhi.

Taarifa  hiyo imeeleza kuwa kukamilika kwa upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 12.9 ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.


Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top