Msichana mrembo ambaye jina lake
halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni aliponea chupuchupu
kubakwa baada ya kuzidiwa na kilevi na kuangukia mikononi mwa wanaume
wakware.
Tukio hilo lilijiri mjini Iringa kwenye
Uwanja wa Samora kulikokuwa na Tamasha la Fiesta ambapo awali msichana
huyo alionekana akicheza kihasara kwa kujigalagaza chini na mzuka
ulipomuishia, alijikokota hadi pembeni akiwa hana nguvu, kitendo
kilichowafanya wanaume wasio wastaarabu kumzingira.
Hata hivyo, walinzi waliokuwa eneo hilo
walitumia nguvu ya ziada kumuokoa mrembo huyo kutoka kwa midume hiyo
iliyokuwa imepania kumkomesha.
Post a Comment