Labda
inawezekana hii ikawa mara yetu ya kwanza kusikia upande wa pili wa
President wetu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae
tumezoea tu kumuona akihutubia, akijumuika na watu mbalimbali kwenye
matukio ya furaha na huzuni lakini kuna mengine hatuyajui kuhusu yeye.
Mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambae ni mbunge wa Chalinze ameongea kwenye Exclusive na millardayo.com na kueleza ni jinsi gani inavyokua pale ambapo baba yake anakasirika au anapokasirishwa akiwa nyumbani.
![Ridhiwani](http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/09/Ridhiwani.png?resize=375%2C226)
‘Yani mtu akimuudhi… huwezi kusikia
amefikia hatua ya kutamka labda huyu mshenziiii…. sina kumbukumbu ya
mimi kumsikia akitamka neno kama hilo, mara nyingi ukikosea anasema huyu
maarifa yake madogo kwelikweli‘ – Ridhiwani
Post a Comment