Taarifa
kutoka kwa maafisa wa polisi zinaeleza kuwa kifo hicho kimetokea baada
ya pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na marehemu Naseeb Langson iliacha
njia na kisha kupinduka na kusababisha dereva kujeruhiwa vibaya na
kufariki muda mfupi baada kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya
Rungwe kwa matibabu.
Taarifa
zaidi zilizoifikia Fichuo Tz zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
mwendokasi wa pikipiki na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika ya
wilaya ya Rungwe.
Pamoja na
hayo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msaidizi mwandamizi wa
polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito
kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na
kuzingatia sheria za usalama wa barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza
kuepukika.


Post a Comment