Mtu mmoja
aliyefahamika kwa majina ya Lughano John aliye na miaka 36 mkazi wa
Ipinda Juu ameuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na
wananchi wenye hasira kali walioamua kujichukulia sheria mkononi baada
ya marehemu kutuhumiwa kuwa ameiba baiskeli.
Tukio
hilo limetokea jana asubuhi ya saa nne katika kitongoji chaLutusyo,
kijijini Talatala katika Tarafa ya Ntebela wilayani Kyela mkoani hapa
Mbeya.
Taarifa
kutoka kwa mashuhuda wa tukio zinaeleza kwamba marehemu Lughano John
alikamatwa na wananchi hao akiwa na baiskeliya wizi na kisha kuanza
kumshambulia kwa kumpiga hali iliyopelekea kifo chake.Wakati
msako wa kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo ukiendelea, Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitishia Fichuo Tz kutokea
kwa tikio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia
sheria mkononi na badala yake wawe na tabia ya kuwapeleka watuhumiwa
wanaokwamatwa katika mamlaka husika.



Post a Comment