Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na mwandani wake Amama Mbabazi.
Kwenye taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa mchango
wake kwa nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi wake Ruhakana
Rugunda ambaye sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao.
Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama
waziri mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara moja.
Waziri mkuu mpya wa Uganda, Daktari Ruhakaan Rugunda anayesubiri kuidhinishwa na bunge.
Waziri mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa angemrithi rais
Museveni lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa huo
uhusiano kati yake na Museveni haujakuwa mzuri.
Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema
kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28 atakuwa
mgombea wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mumewe ameonewa.
Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.
(CREDIT: BBC SWAHILI)
on Saturday, September 20, 2014
Post a Comment