Watafiti wamechanganyikiwa kuhusu ikiwa
kampuni ya Apple inapaswa kutoa kauli yake kuhusu ripoti kuwa simu yake
mpya ya iPhone 6 inajipinda mtumiaji anapoishi kuiweka ndani ya mfuko wa
suruale yake.
Watu kadhaa ambao ni watumiaji wa iPhone 6 wamekuwa wakituma picha zao kwenye mtandao wa MacRumors ambazo zineonekana kuonyesha simu zao zikiwa na tatizo hilo.
Mwandishi wa habari kwenye mtandao wa 'Geek.com' pia aliripoti kuwa simu yake ye iPhone 6 imejipinda.
Na haijulikani nini hasa kinachoifanya simu hiyo kujipinda, baadhi wakisema huenda ni gamba lake ambalo limetengezwa kwa madini ya Aluminium ambalo linaifanya rahisi kwa simu hiyo kujipinda.
Taarifa za iPhone 6 kujipinda hazijaripotiwa tu kwenye blogu za habari za kiteknolojia bali pia kwenye vyombo vya habari kama Independent, the Washington Post, India Today na the Sydney Morning Herald.
Post a Comment