Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ akiwa mikononi mwa Polisi.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a
Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ hivi karibuni alilala katika Kituo
cha Polisi cha Kigamboni, Dar akihusishwa na utekaji wa dereva wa
bodaboda, Suedi Waziri (pichani) kisha kumpa kipigo ambapo inadaiwa
alisoteshwa kinomanoma.
Baada ya tukio hilo lililotokea mwishoni
mwa wiki iliyopita, Ijumaa lilinasa picha zinazomuonyesha msanii huyo
akihenyeshwa kituoni hapo huku mmoja wa watu wanaoishi karibu na eneo
hilo akinyetisha kuwa, licha ya ustaa wake Madee alikiona cha mtemakuni.
Dereva wa bodaboda, Suedi Waziri aliyetekwa na kushambuliwa na Madee.
“Mimi nilikuwepo pale kituoni,
nilimshuhudia akiwa amepigwa pingu huku polisi kama sita hivi, mmoja
akiwa na silaha wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi wakimpeleka
mahakamani.“Alionekana aliyechoka sana huku akiwa na hofu ila
inavyodaiwa baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakihaha kumnusuru
baada ya kulala selo,” kilidai chanzo hicho.
Majeraha ya mguuni aliyopata Suedi Waziri baada ya kushambuliwa na Madee.
Kufuatia msala huo, msanii huyo
alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kigamboni na baadaye kuwekewa
dhamana na baba yake ambapo kesi yake itatajwa tena Oktoba 6, mwaka huu.
Madee anadaiwa kumteka Suedi na kwenda
kumsulubu nyumbani kwake Manzese baada ya kijana aliyekuwa amepakia
kwenye bodaboda yake kukwapua simu ya msanii huyo na kukimbia.
Katika kushinikiza simu yake irudishwe
ndipo Madee alipomtaiti Suedi na mwisho wa siku akaishia mikononi mwa
polisi kwa kufunguliwa kesi iliyosomeka: VJB/RB/625/2014 KUTEKWA KWA BINADAMU
Post a Comment