Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAHAKAMA YAWAACHIA KWA DHAMANA VIONGOZI WA CHADEMA WALIOSOTA MAHABUSU

 

Hatimaye mahakama ya wilaya ya bunda mkoani mara imewachia kwa  dhamana viongozi na wanachama kumi wa chama cha Demokrasia na  maendeleo Chadema baada ya kusota mahabusu kwa siku sita kufuatia  kesi ilifunguliwa na jeshi la Polisi kwa kudaiwa kufanya mkusanyiko  kinyuime cha sheria na kuhatarisha amani.
Wakizungumza muda mfupi baada ya viongozi hao sita wakiwemo  wanachama wanne wa Chadema na CCM kupata dhamana hiyo kwa  kusimamiwa na mawakili kutoka kampuni ya mawakili ya Ap ya jijini Mwanza, viongozi baadhi ya Chadema mkoa wa Mara na wilaya ya  Bunda, wamedai kusikitishwa na nguvu kubwa zinatumiwa na vyombo  vya dola dhidi ya vyama vya upinzani. 
 
Hata hivyo mmoja ya mawakili hao kutoka katika kampuni ya uakili ya Ap ya jijini Mwanza Bw Afred Goyayi ameishukuru mahakama hiyo ya wilaya ya Bunda kutenda haki kwa kukubali maombi ya dhamani kwa   watuhumiwa hao baada ya upande ya mashitaka kuweka pingamizi  kuhusu dhamana hiyo. 
 
Septemba 23 mwaka huu jeshi la Polisi liliwakamata viongozi na  wanachama hao wa Chadema na CCM kwa madai ya kufanya  maandamano ambayo yalizuiwa na jeshi la Polisi kisha kufunguliwa  mashitaka ya kufanya mkusanyiko bila kibali kinyume cha sheria na  kuhatarisha amani, kesi hiyo imepangwa kutajwa tena mahakamani hapo oktoba saba mwaka huu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top