Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AMIGOLAS WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA .... hivi ndivyo ilivyo msibani kwa sasa


Mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI wa  zamani wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’  amefariki duniabaada ya kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku kadhaa.
Amigo alilazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa upasuaji zilikuwa zikiandaliwa lakini mauti yakamkuta kabla ya lolote kufanyika.

Mwimbaji huyu ambaye hadi anafariki, alikuwa mtumishi wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Amigo alikuwa mmoja wa wanamuziki waasisi wa Twanga Pepeta, akaitumikia kwa uaminifu mkubwa kwa miaka mingi kabla ya mwanzoni mwa mwaka huu yeye na wenzake kadhaa kuanzisha Super Stars Band ambayo baadae ikachukuliwa na JKT na kuwa Ruvu Stars Band.
Akiwa Twanga Amigo akajijengea umaarufu wa aina yake na kuwa kama moja ya nembo ya bendi, katika utumishi wake uliotukuka ndani bendi hiyo, akafanikiwa kutunga wimbo mmoja 'AMINATA'  ambao ulikamata chati kwa miaka mingi tangu ulivyorekodiwa mwaka 2003.
Kufariki kwa Amigo ni pengo kubwa kwa Ruvu Stars hasa kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye alikuwa

‘injinia’ wa mipango yote kuanzia Super Stars hadi Ruvu.
Kabla ya Twanga Pepeta, Amigo aliitumikia pia bendi ya Bicco Stars chini ya Kinguti System.

Msiba uko nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu Mburahati jijini Dar es Salaam jirani kabisa na Shule ya Msingi Mianzini na taratibu za mazishi zinasubiri ndugu na jamaa kutoka Tabora na Kigoma.Chanzo GPL
!
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa msibani.Rogert Hega, 'Katapilla' akiwa msibani.Victor Mkambi akiwa msibani.Mama mzazi wa marehemu, Aisha Suleiman, akilia kwa uchungu.Mtoto wa marehemu, Sophia Khamisi akiwa amezimia msibani.Waombolezaji wakiwa msibani.Waombolezaji wengine wakimfariji mke wa marehemu aliyelala(katikati).Waimbaji wenzake na marehemu Amigolas wakijadili utekelezaji wa mazishi ya mwenzao.MAZIKO ya mwanamuziki wa zamani wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ aliyefariki usiku wa kuamkia leo yatafanyika kesho saa 9 alasiri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. 


Amigolas amefariki kwa ugonjwa wa moyo akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa. Mwimbaji huyu ambaye hadi anafariki, alikuwa mtumishi wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Amigo alilazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa upasuaji zilikuwa zikiandaliwa lakini mauti yakamkuta kabla ya lolote kufanyika. 
Marehemu Amigolas amefariki akiwa na umri wa miaka 42, ameacha mke na watoto wanne, watatu wa kike na mmoja wa kiume. Msiba upo nyumbani kwa mama wa marehemu, Mburahati, Mianzini jijini Dar. 
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. AMEN!
 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top