Wahitimu
wa kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013
waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi baada ya usaili kukamilika
Maelekezo Muhimu.
Wahitimu
wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT
Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea,
Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro,
Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi
la Polisi.
Wahitimu
hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda
wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili
waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe
30/11/2014.
Zoezi
la usajili litaanza shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe
15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.
Atakaeamua
kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika
kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania mjini Moshi.
Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
Vyeti
vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip
pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa
(Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
Chandarua chenye upana futi tatu
Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).
Pesa kidogo ya kujikimu.
Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo.
on Monday, November 10, 2014
Post a Comment