Tumekua
tukizipata taarifa za watu mbalimbali kukamatwa na dawa za kulevya
kwenye viwanja vya ndege pamoja na sehemu nyingine za kusafirishia
ambapo kila mmoja amekua na mbinu yake kusafirisha mzigo huo haramu.
Stori
mpya ya leo imetokea Nigeria ambapo mwanaume aitwae Mama Solomon kutoka
Enugu amekamatwa kwenye uwanja wa ndege Lagos akiwa ameficha dawa za
kulevya aina ya Cocaine katikati ya soli ya kiatu cha Mwanamke.
Jamaa
alikua akitokea Brazil ambayo ni nchi maarufu sana kwa kuziuzia nchi
nyingine dawa za kulevya na alikua na mifuko miwili iliyojaa viatu vya
Wanawake na pochi.
Baada
ya kukamatwa, Solomon mwenye umri wa miaka 27 alikataa dawa hizo kuwa za
kwake na kusema yeye amekua akifanya kazi na kuishi nchini Brazil hivyo
kuna rafiki yake alimpatia huo mzigo na kumwambia akiufikisha salama
atazawadiwa.




Post a Comment