
Mama
mzazi wa Wema Sepetu, Miriam SepetuHII ni mara yangu ya tatu nazungumza
na mama mzazi wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu juu ya mwenendo wake kwa
mwanaye, ambaye ana simulizi nyingi zinazomhusisha na mambo yaliyo nje
ya fani yake ya uigizaji.
Wakati
ule, ilikuwa ni juu ya tabia yake ya mara kwa mara ya kulizungumzia
penzi la Wema na Diamond, kabla wawili hao hawajaachana kwa mara ya
kwanza. Alikuwa akimpinga waziwazi kijana yule wa Tandale, kwa madai
kuwa anampotezea muda mwanaye na mambo mengine kama hayo.
Nilijaribu
kumweleza kwa jinsi gani ilikuwa haipendezi kwake kufuatilia sana mambo
ya kimapenzi kwa watoto, maana ingawa anayo nafasi kubwa, lakini aina
ya maisha ya siku hizi yanatoa nafasi kubwa zaidi kwa wahusika kuliko
wazazi.Lakini wakati akijipongeza kwa kufanikisha kuachana kwa wawili hao, ghafla wakarudiana na kumfanya mama mtu kuaibika, kwani ilionyesha wazi mwanaye alikuwa bado ana mapenzi kwa Baby wake, Diamond Platinumz.
wazazi.Lakini wakati akijipongeza kwa kufanikisha kuachana kwa wawili hao, ghafla wakarudiana na kumfanya mama mtu kuaibika, kwani ilionyesha wazi mwanaye alikuwa bado ana mapenzi kwa Baby wake, Diamond Platinumz.
Na mara
ya pili nilisema naye wakati alipomtukana matusi makubwa ya nguoni shoga
wa zamani wa mwanaye, Kajala Masanja, katika sherehe ya kumbukumbu ya
kuzaliwa kwa mtoto wake. Ni matusi ambayo licha ya kuwa hayaandikiki
gazetini, lakini pia nilimweleza jinsi gani alivyokosa busara za mzazi
kwa kutamka maneno mazito kama yale, mbele ya watoto! INAENDELEA>>


Post a Comment