ASKARImmoja
kati ya watatu waliokuwa wakituhumiwa kwa mauaji kwa aliyekuwa mwanafunziwa
Chuo kikuu TEKU, amehukumiwa kunyongwa hadi kufa huku wenzie wakiachiwahuru.
Hukumuhiyo
ilitolewa katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya na Jaji Rose Temba baada
yakuridhishwa na ushahidi wa pande zote mbili uliotolewa mahakamani hapo
kwanyakati tofauti.
Mwendeshamashtaka
wa Serikali, Archiles Mulisa akisaidiwa na Catherine Paul aliwatajawashtakiwa
kuwa aliyehukumiwa ni Askari polisi F5842DC Maduhu na walioachiwa ni pamoja
na F 7769 DC Shaban na WP 6545 DC Neema baada yakuwakuta hawana hatia.
Mtuhumiwahuyo
amepatikana na kosa hilo kwa mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu chaTeofilo
Kisanji(TEKU) Daniel Mwakyusa aliyekuwa mwaka wa kwanza wa masomo mwaka2012.
Hukumu hiyo
ya imetolewa na jaji Rose Temba baada ya kuridhishwa na
ushahidiuliotolewa na pande zote mbili.
Awali
ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali Archiles Mulisa akisaidiwa
naCatherine Paul kuwa washitakiwa wenyekesi namba 16 ya mwaka 2013
walifanya mauaji ya kukusudia mnamo Februari 14mwaka 2012 kinyume cha kifungu
namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kamailivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Wakili
Mulisa alisema washitakiwa hao kwa pamojawalihusika na mauaji ya Daniel
Mwakyusa baada ya kumpiga marehemu huyo kwakutumia silaha inayodhaniwa kuwa ni
bunduki nje ya ukumbi wastarehe ujulikanao Univesal uliopo Uyole jijini
Mbeya.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo,jaji Temba alisema anawaachia huru mshitakiwa namba
mbili DC Shaban ambaye alikuwadereva wa gari ya polisi kwakuwa ushahidi
uliotolewa unadhihirisha kuwa alibakindani ya gari akimsubiri mshitakiwa namba
moja aliyeshuka na kuingia kwenye bar hiyo.
Kwa upande wa mshitakiwa namba tatuDC Neema,Jaji Temba alisema aliridhishwa na
mshitakiwa huyo kutohusika namauaji kwakuwa siku ya tukio alikuwa akijisikia
vibaya hivyo alilazimika kubakina dereva kwenye gari.
Jaji Temba alisema mshitakiwa nambamoja DC Maduhu anahusika moja kwa moja na
mauaji hayo kutokana na ushahidi wakimazingira kwani yeye ndiye aliyekuwa mtu
wa mwisho kuondoka na marehemu eneola tukio na kumpeleka kwenye gari.
Alisema sababu ya pili,ushahidiulionesha kuwa silaha yake pekee ndiyo
iliyotumika tofauti na za askari wenginekwakuwa risasi tatu zilionekana
kupungua kati ya zile alizokabidhiwa sambambana ushahidi wa maganda matatu ya
risasi yaliokotwa eneo la tukio.
Aidha,Jaji Temba alisema sababu yatatu ni kuwa ushahidi uliotolewa unaonesha
kuwa mshitakiwa huyo alikuwa wamwisho kurejesha silaha hivyo kuhusishwa moja
kwa moja na mauaji hayo.
Alisema kutokana na sabvabu hizomahakama inamtia hatiani kwa kuua kwa kukusudia
hivyo mshitakiwa DC Maduhuamehukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Awali ilidaiwa kuwa siku ya tukioilikuwa siku ya wapendanao(Valentine Day)
ambapo mtuhumiwa akiwa doria naaskari wenzie alimkuta marehemu akiwa kwenye
eneo la starehe na mwanamke anayesadikiwakuwa alikuwa pia na mahusiano na
askari huyo.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
Post a Comment