PROF. MUHONGO
MH.WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
- Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini amekuwa, mara
kwa mara, akilipotosha Bunge tukufu na Taifa kwa ujumla kuhusiana na
Fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na
fedha za umma. Hata mtu wa kawaida angeweza kujua kwamba washirika wa
‘Tegeta Escrow Account’ ni akina nani na masharti ya kutoka kwa fedha
hizo kwenye akaunti ni yapi
kwa mujibu wa Mkataba wa uendeshaji wa akaunti hiyo.
-Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, aidha kwa makusudi ama kwa
sababu anazozijua vizuri zaidi mwenyewe, Waziri wa Nishati ananukuliwa
kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge, Kwa nguvu
kubwa na kwa kujiamini, akitetea uchotwaji wa fedha hizo kinyume na masharti ya Mkataba wa Escrow.
-Aidha, Kamati imebaini kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye
alikuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi na
Bwana James Rugemalira, tena katika ofisi ya Umma; na
pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa
Nishati na Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa Bwana Sethi
hana uhalali wa kisheria kufanya biashara kwa jina la IPTL.
-Iwapo Waziri wa Nishati na Madini angetimiza wajibu wake ipasavyo,
Fedha za Tegeta ESCROW zisingelipwa kwa watu wasiohusika, na Nchi
ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea kama kodi za VAT,
Capital Gain Tax na Ushuru wa Stempu ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 30.
-Kamati inapendekeza kuwa Mamlaka yake ya uteuzi itengue uteuzi wa
Waziri wa Nishati na Madini kutokana sababu hizo zilizoelezwa.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
-Kamati imethibitisha kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini alisema
uongo Bungeni kwa kutamka kauli ambazo zilizokuwa na lengo la kupotosha
umma kuhusu akaunti ya Tegeta ESCROW ikiwemo kutoa
kauli ambazo zingeweza kusababisha Nchi kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na
nchi ya Uingereza.
-Kamati inapendekeza kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini
achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwemo kutenguliwa uteuzi wake.
Kamati pia inapendekeza kuwa Naibu Waziri huyu afikishwe mbele ya
Kamati ya Bunge ya Maadili ili aadhibiwe kama Mbunge kwa kusema
uwongo Bungeni ili liwe fundisho kwa wabunge wengine kuhusiana na kauli
wanazotoa ndani ya Bunge lako tukufu.
KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
-Kamati imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
aliingia makubaliano ya kutoa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW
bila kujiridhisha kikamilifu kuwa maamuzi ya hukumu ya ICSID 2 yalikuwa
bado kutolewa na hivyo kusababisha fedha kutolewa bila kukokotoa upya
gharama za ‘capacity charges’, jambo ambalo limesababisha kupoteza fedha
za umma.
-Vile vile, Kamati imebaini kuwa, Katibu Mkuu hakufanya uchunguzi wa
kina (due diligence) kujiridhisha uhalali wa Kampuni ya Mechmar kuuzwa
kwa Piperlink na baadaye kuuzwa kwa PAP, na hivyo kusababisha fedha za
akaunti ya Tegeta ESCROW kulipwa kwa asiyestahili na kinyume cha Mkataba
wa akaunti ya Escrow.
-Kwa maana hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, pengine
kwa uzembe wake ama kwa kukusudia kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe
zaidi, amesaidia uchotwaji na
hatimaye utakatishaji wa fedha haramu.
-Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali ya juu uliofanywa na Katibu
Mkuu huyo, kushindwa kujiridhisha kama masharti ya Sheria ya kodi ya
Mapato Sura ya 333, Kifungu cha 90(2) yalitekelezwa. Kifungu hicho
kimsingi kinaitaka mamlaka ya ‘approval’’ ya uhamishaji wa Makampuni
kutotambua Kampuni mpaka kwanza kodi za uhamishaji ziwe zimelipwa na
hati za malipo ya kodi zimetolewa na mamlaka ya kodi.
-Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Katibu Mkuu huyu utenguliwe, na
TAKUKURU wamfikishe mahakamani mara moja, kwa kuikosesha Serikali
Mapato, matumizi mabaya ya ofisi na kusaidia utakatishaji wa fedha
haramu.
KUPATA RIPOTI KAMILI YA PAC KUHUSU ESCROW INGIA: HAPA
KAMATI YA PAC YAMTAKA WAZIRI MKUU, MWANASHERIA MKUU, WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WAWAJIBIKE KUHUSU RIPOTI YA TEGETA ESCROW
Post a Comment