Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote
(Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji
Aliko Dangote akitumia gari kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda
chake kikubwa cha saruji katika Kijiji cha Msijute, mkoani Mtwara
leo.
Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote
(Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji
Aliko Dangote (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Dangote
nchini, Esther Baruti kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo.
Ndege ya bilionea huyo wa Afrika, Alhaji Dangote ikitua kwenye
Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Alhaji Aliko Dangote kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi
Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti alipowasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Mtwara leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA
MATUKIO BLOG
Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Manjanbu akimlaki Alhaji
Dangote.
Dangote akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Kampuni yake hapa nchini,
Esther Baruti
Dangote akikaribishwa na viongozi wa kampuni ya Dil & Sinoma
alipowasili eneo la Kiwanda cha simenti cha Dangote.
Alhaji Dangote akiwa na maofisa wake katika kikao na
viongozi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma kwa
ajili ya kupewa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho
ambacho kitakuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.
Waandishi wa habari wakimhoji Dangote kuhusu maendeleo ya ujenzi
wa kiwanda hicho
Alhaji Aliko Dangote
Alhaji Dangote akiwa kwenye msafara wa magari akikagua maendeleo
ya ujenzi ya kiwanda cha saruji Mtwara
Mwakilishi Mkazi wa Kampuni hiyo ya Dangote hapa nchini, Esther
Baruti akiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Dangote
Alhaji Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenda nchini
Ethiopia kuendelea na ziara yake
Ofisa Mnadhimu wa Poilisi Mkoa wa Mtwara, George Salala akiagana
na Alhaji Dangote
Alhaji Dangote akipanda ndege tayari kuondoka kwenye Uwanja wa
Ndege wa Mtwara
Mwakilishi Mkazi wa Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiondoka
baada ya kuagana na Dangote
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote ikipaa
Post a Comment