Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Taarifa Kwa Umma Kutoka Makao Makuu ya Jeshi La Wananchi wa Tanzania Kuhusu Kifo Cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (Mstaafu)

 Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) enzi za Uhai wake
---
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange anasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) kilichotokea tarehe 29 Oktoba 2014 katika Hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa akipata matibabu.

Mwili wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo. 
  Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.
Imetolewa na
 Kurugenzi ya Habari na Mahusiano Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top