
Tanzania imeshtushwa na ripoti inayoelezea biashara haramu ya meno ya tembo kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China
Serikali
ya nchi hiyo imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya
uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa kichina
wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania ndio
wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya meno ya
tembo.
Inadaiwa kwamba raia wa China walitumia ziara ya rais wao nchini humo kusafirisha kimagendo maelfu ya kilo za pembe za ndovu.
Kulingana
na shirika la utafiti wa mazingira, EIA, Pembe hizo zilinunuliwa wiki
moja tu kabla ya ziara ya rais huyo nchini tanzania mwaka jana na
zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili zisitambuliwe.
Msemaji
wa serikali Assah Mwambene amemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar famau
kwamba ripoti kama hiyo zinatatiza jitihada za serikali kukabiliana na
uuzaji haramu wa pembe za ndovu.Chanzo BBC Swahili


Post a Comment