Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Watu wanne waliomuua Albino wahukumiwa kunyongwa mkoani Geita.


Mahakama kuu ya Tanzania katika kikao chake kilichofanyika mkoani Geita imewatia hatiani na kuwahukumu kunyogwa mpaka kufa, watuhumiwa wa nne wa mauaji ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi Zawadi Magindu aliyeuwawa mwaka 2008 katika kijiji cha Nyamalulu wilayani.
Kwa kuzingatia ushahidi na utetezi wa pande zote jaji Joaquine De-mello amesema mahakama imejiridhisha pasipo kuacha shaka yoyote kuwa watuhumiwa wote wanne walihusika na mauaji ya Bi Zawadi Magindu katika kijiji cha Nyamalulu wilayani Geita mnamo tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka 2008 usiku.
 
Kwa mujibu wa mashahidi waliojitokeza inasemekana mtuhumiwa namba mbili Ndahanya Lumola na mtuhiwa namba tatu Singu Siantemi ndio waliohusika na upimaji wa mifupa ya marehemu Zawadi ambapo hutumia wembe na shilingi moja kuweka karibu na mifupa ya Albino ili kujua kama itavuta kama sumaku na kipimo kingine ni redio ambayo huiweka karibu na mifupa na ikizimika ndio mifupa hiyo huonekana kuwa na ubora tofauti na hapo mifupa hiyo huwa haifai na hutupwa.
 
Mashahidi hao wamesema vipimo hivyo havina uhalisia wa aina yoyote kwani hakuna binadamu mwenye mifupa inayokuwa na sumaku.
 
Aidha jaji De-mello amesema anashangazwa na kesi zote alizosimamia zinazohusu mauaji ya Albino watuhumiwa wote wanaofikishwa mahakamani ni wakataji wa mapanga na kuhoji wakataji hao wanapeleka wapi mifupa hiyo? Na kuwataka wahusika kuhakikisha wanawapata wanunuzi na watumiaji wa viongo hivyo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.
   
Watu waliokutwa na hatia ya kufanya mauaji hayo ni Masalu Kahindi, Ndahanya Lumola, Singu Siyantemi na Nassoro Saidi ambaye ni mume wa marehemu Zawadi.
 
Kwa upande wao watu wenye ulemavu wa ngozi wameipongeza mahakama kwa kutoa hukumu ya haki inayoashiria kuwapa ulinzi jamii hiyo ya maalbino.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top