Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SAIDI FELLA AFICHUA SIRI ILIYOJIFICHA, YAMHUSU ASLAY NA KUNDI ZIMA LA YAMOTO BAND



Aslay and Fella
Fela ametoa maneno hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook wakati akimpongeza Dogo Aslay katika siku yake ya kuzaliwa. Mkubwa Fela akampa usia mzito Dogo Aslay pamoja na kumshukuru na kumpongeza kwa juhudi za ushirikiano wake uliosaidia kuisimamisha vilivyo Mkubwa na Wanawe pamoja na Yamoto Band.

Katika maandishi yake hayo, Fela akafichua kuwa ujenzi wa nyumba za waimbaji wote wanne wanaounda Yamoto Band uko ukingoni na panapo majaaliwa watakabidhiwa mwezi Julai mwaka huu. 

Mtaandao huu unakuwekea maneno yote ya Said Fela neno kwa neno bila kuongeza wala kupunguza kitu na baada ya hapo kiroho safi kabisa tumpe pongezi zake. 
Happy birthday mwanangu Aslay Isihaka mwanangu sina cha kukuusia ila MUNGU alishakupa Imani na upendo ila natakiwa nikuongoze na mafanikio yako wadau wayaone nikitamka ivi kama ada yangu kwenye moyo wangu. Nilikushauri kusapot wenzio hukubisha mpaka tumetengeneza Yamoto Band mpaka leo umefunga pini mpaka umewatobolesha wenzako Beka, Maromboso na Enock Bella pia kukitambulisha kituo chetu cha Mkubwa na Wanawe nchini na kwenginepo duniani. Najua kuna wadau wanapenda kujua mpaka sasa umefaidika nini wewe napenda kuwafamisha japo upendagi, ulisomeshwa na Mkubwa Fela na ulipata nyumba ya kwanza 2013. Na tangu tuiazishe Yamoto Band ulitoa wazo ulisema mkubwa kama unavyojua familia tulipotokea naomba tutengenezee kota zetu zifanane ata tukizeeka tuwakumbuke. Asante wazo lako tumelifanyia kazi ujenzi unafikia mwisho na INSHAALLAH tunafanya mipango mimi na viongozi wenzangu wa Mkubwa na Wanawe Youth Centre tumpate mh raisi wetu wa jamhuri ya Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE mwezi wa 7 awakabidhi nyote Yamoto Band nyumba zenu, muhimu tuombe dua INSHAALLAH happy birthday Aslay.
Yamoto BandYamoto Band Kutoka kushoto ni Enock Bella, Maromboro, Dogo Aslay na Beka One
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top