Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amemshambulia Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kwamba vinatumiwa na wabaya wake kumkashifu katika utendaji wake.
Profesa
Tibaijuka alitoa shutuma hizo wakati akihutubia wananchi wa Kata ya
Bureza. Alisema alikumbwa na kashfa ya Escrow, kutokana na kupata fedha
kutoka kwa kaka yake Rugemalila (James) alizompa kusaidia shule
anayoisimamia.
Alikanusha
tuhuma zilizotolewa na Mdee bungeni dhidi yake kwamba alipokuwa Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kabla ya kuvuliwa wadhifa huo,
alikuwa mporaji wa mali za wananchi hasa kumiliki ardhi kubwa.
Alidai
kuwa katika kashfa hiyo, kitendo cha kusema fedha aliyoipata ni ya
mboga kwa maana ni ndogo imetafsiriwa na kutumiwa na vyombo vya habari,
hasa magazeti kumchafua zaidi ndani na nje ya Tanzania.
“Nasema
hapa mbele yenu na waandishi wa habari wapo hapa, magazeti yanafanya
biashara kupitia kwangu kwani wanapoandika habari zangu magazeti
yananunulika kwa haraka siku husika,” alisema Profesa Tibaijuka.
Alidai
kuwa Mdee alidanganya bungeni kuwa Profesa Tibaijuka ni mporaji ardhi
za wananchi kuanzia jimboni na kama isingekuwa ni kinga ya mbunge
kutoshtakiwa, angemfungulia mashtaka mahakamani.
Alisema
waandishi wa habari hawaandiki mambo mema aliyofanya jimboni badala
yake wamesimama kwenye kashfa ya Escrow lakini yeye hafanyi maendeleo
yake kwa fedha hizo, bali ana pensheni ya Umoja wa Mataifa (UN).
“Fedha
nilizopata Umoja wa Mataifa bado ninazo na Halima Mdee tutakuja
kukutana mbele ya safari kama ni pesa ya kula bado ninayo na ile ya
Escrow ya Rugemalila ni kuhemea mboga acheni kudanganyika,”alisema Profesa Tibaijuka.
Aliwaomba
wananchi wa kata hiyo kumuunga mkono kwani licha ya kudaiwa kuwa ana
umri mkubwa hivyo awaachie vijana, bado yumo na atagombea tena
kuwaongoza wananchi akiwa mbunge.
Akijibu shutuma dhidi yake Mdee alisema alichokisema ni cha kweli na kwamba anao ushahidi kuthibitisha madai yake hayo.
“Asiweweseke kwa kuwa hilo suala la uporaji wa ardhi ni la kweli na wala sikumuonea.”
“Asiweweseke kwa kuwa hilo suala la uporaji wa ardhi ni la kweli na wala sikumuonea.”
Post a Comment