Chama
cha ACT-Wazalendo kimesema kimekuwa na mawasiliano na Dk. Wilbrod Slaa,
kuhusu uwezekano wa yeye kushiriki katika kampeni za Chama chao kwa
lengo la kuendeleza vita dhidi ya ufisadi nchini.
Katibu
Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba anasema kuwa Dk. Slaa
ilikuwa afanye nao mikutano ya kampeni katika maeneo tofauti ya Tanzania
"Dr.
Slaa alikuwa aanze na Mkutano wa hadhara Mjini Iringa siku ya Jumatano
tarehe 7 Oktoba 2015, na baadaye angeendelea na mikutano mingine katika
majimbo mbalimbali na kuhitimisha kampeni hizo katika Viwanja vya
Mwembeyanga Jijini Dar es Salaam, ambao ndio uwanja ambapo vita dhidi ya
ufisadi ilitangazwa rasmi mnamo tarehe 15 Septemba 2007" Alisema
Mwigamba
Katibu
mkuu huyo wa ACT Wazalendo ameongeza kuwa"Baada ya tathmini ya kina
chama cha ACT-Wazalendo kimejiridhisha kwamba hali ya usalama wa Dkt
Slaa ni ndogo sana kwa sasa kutokana na vitisho mbalimbali anavyovipata.
Kutokana na hali hiyo ya vitisho dhidi ya usalama wake, chama chetu
kimejiridhisha kuwa hakina uwezo wa kumhakikishia Dk. Slaa usalama wake
atakapokuwa majukwaani.
Kwa
kuzingatia maelezo ya hapo juu, chama chetu kimefuta mikutano yote
ambayo Dk. Slaa alikuwa aifanye kupitia jukwaa la ACT-Wazalendo. Chama
kitaendelea kutambua mchango wake katika harakati za kukuza demokrasia
na hasa bidii yake ya kujitoa katika kupambana na ufisadi nchini.
Tunamuahidi kwamba chama chetu kitaendeleza vita hii kwa bidii kubwa na juhudi zake kamwe hazitapotea" . Amesema Mwigamba
Post a Comment