Mgombea
Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
kinachoungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA Edward Lowassa
amesema Sera yake anayoitumia ya Elimu kwanza si kwa mfumo uliopo sasa
bali atabadilisha mfumo mzima na kuufanya kuwa wa TEKNOHAMA.
Amedai
teknolojia hiyo ataifanya iweze kuwafikia wananchi kwa wepesi kwa
kutumia rasilimali zilizopo kama Gesi asilia, madini ,vyanzo vya utalii
na fedha zilizopo kwa kuwa anaamini Serikali bado ina pesa nyingi.
Akiwahutubia
wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika Viwanja vya Mwembe Yanga
vilivyopo katika Manispaa ya Temeke amesema kutokana na uwezo wake iwapo
akipata dhamani, Serikali yake itakuwa na kasi na watakaoshindwa
kuimudu itabidi wampishe.
Naye
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya Tatu Fredrick Sumaye amesema, uamuzi
wao wa kujitoa ndani ya CCM ulitokana na kuamini kuwa walioko CCM ni
mafisadi.
Zikiwa
zimebaki siku 23 kabla ya uchaguzi mkuu mgombea huyo amefanya ziara
zake katika maeneo ya Temeke, Tabata, Sinza – Ubungo na kuhitimisha
kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe mkoani Dar es Salaam.
Post a Comment