Aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, Kassim Kayira.
Aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, Idd Seif
.(P.T)
Kassim Kayira na Idd Seif wakiwa katika studio ya BBC.
Idd Seif na Kassim Kayira wakiagana.
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC wakiwaaga watangazi hao.
WATANGAZAJI bora
kabisa wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, katika kipindi cha
Dira ya dunia, Kassim Kayira na Idd Seif wameacha kazi katika kituo
hicho kikubwa duniani.
Kwa
mujibu wa watangazaji hao wawili waliokuwa pamoja studio katika kipindi
cha Dira ya Dunia kwa mara ya mwisho jana, walisema wameamua kuacha kazi
na kurudi nyumbani Afrika ili kuendeleza miradi yao.
Idd Seif,
ambaye alijiunga na BBC mwaka 1997 akitokea Kampala, Uganda, alisema
ameamua kurejea Uganda ili aweze kusimamia miradi yake, baada ya kazi ya
utangazaji kwa miaka 40. Alielezea huzuni yake kwa kuwaacha watu
waliompokea vizuri na kufanya nao kazi kwa miaka 20.
Kwa
upande wake, Salim Kayira, alisema alijiunga na shirika hilo akitokea
kituo cha televisheni cha Rwanda miaka kumi iliyopita akiwa Mhariri.
Alisema naye atarejea Afrika ambako atajishughulisha na kilimo pamoja na
ufugaji na sehemu aliyoamua kuishi ni Uganda.
Watangazaji
hao wameondoka miezi michache baada ya mtangazaji mwingine mahiri wa
Kiswahili, Charles Hilary wa Tanzania kuacha kazi na kujiunga na kituo
cha televisheni cha Azam. Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinasema
wawili hao nao huenda wakajiunga na Azam tv.
Post a Comment