Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HUSSEIN BASHE AWACHANA UKAWA

Hassan Kibiki's photo.
MGOMBEA ubunge wa CCM katika Jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe, amesema wapinzani wanataka kuwagawa wananchi kwa misingi ya udini na ukabila.
Akihutubia katika mkutano wa kampeni katika mji wa Ndala wilayani Nzega alisema kwa miaka mingi watanzania wameishi kwa umoja bila kujali ukabila na udini, lakini wapinzani wanataka kuleta mambo hayo kwa lengo la kuwagawa Watanzania. “Hawa wanakuja kutugawa kwa ukabila na udini, msikubali kugawanywa kwa misingi ya udini na ukabila, ichagueni CCM tuendelee kubaki wamoja,” alisema Bashe. Mgombea huyo ambaye anafahamika kuwa mtu wa karibu na mgombea urais wa Lowassa kutokana na kuwa msemaji wa Kambi ya Lowassa wakati wa mchakato wa kusaka urais kwa tiketi ya CCM, alisema mabadiliko yanayohubiriwa na wapinzani yameshafanywa na CCM. “Vijana wenzangu nawaombeni kama ni mabadiliko tuyatafute ndani ya CCM, wanasema eti CCM ni ile ile haifanyi kitu, mimi nawaambia CCM ni ile ile ila madereva tofauti. “Safari hii dereva ni Magufuli, kondakta ni Mama Samia na sisi akina Bashe, Kigwangala (Hamisi) ni mautingo na safari itakuwa salama,” alisema Bashe.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top