Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Lowassa aahidi kudhibiti tatizo la mgao wa umeme nchini

Mgombea wa nafasi ya kiti cha urais kupitia tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Edwrad Lowassa ameahidi kuthibiti tatizo la mgao wa umeme ambao umekuwa changamoto kubwa kwa wananchi.

Mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa ametoa ahadi hiyo huku akionekana dhahiri kuchukizwa na ahadi zisizotekelezeka za kutatua kero hiyo ya umeme ambapo amesema serikali atakayoiunda itahakikisha inadhibiti kikamilifu suala la mgao wa umeme.
 
Mgombea huyo anayeungwa mkono na asilimia kubwa ya vijana ambao ni zaidi ya asilimia 65 kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, ametumia jukwaa hili la mkutano wa hadhara hapa Same kutoa onyo kwa shirika la umeme nchini Tanesco.
 
James Mbatia mwenyekiti wa NCCR mageuzi amesema umasikini wa watanzania unachochewa na uongozi mbovu wa CCM ambao umekuwa ukitumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya kundi dogo la watu wachache.
 
Katika siku yake ya kwanza ya kampeni mkoani Kilimanjaro amehutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Hedaru, Ndungu, Same na Mwanga ambapo pia alipata fursa ya kuweka shada la maua katika kaburi la muasisi wa CCM Peter Kisumo mjini Usangi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top