Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mabadiliko ya Tume ya taifa ya Uchaguzi, yapigiwa kelele



Mtandao wa Asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO leo umeeleza kushtushwa kwake na mabadiliko yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya tume ya taifa ya uchaguzi NEC huku wakisema kuwa mabadiliko hayo hayana ishara nzuri kwa watanzania hususani kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam Kaimu mwenyekiti wa TACCEO wakili IMELDA LULU URIO amesema kuwa mabadiliko yanayofanywa kwa sasa ni makubwa sana kufanyika katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kwa chombo chenye dhamana ya kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi na kuhakikisha ushiriki wa wananchi katika kupiga kura.

Amesema kuwa kwa siku ya hivi karibuni imeshughudiwa mabadikilo makubwa ya baadhi ya watendaji na makamishna wa tume hiyo huku akitolea mfano mabadiliko yaliyofanyika tarehe 25 mwezi wa 7 mwaka huu ambapo rais KIKWETE alifanya mabadiliko kwa kumuondoa aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya siku ya kupiga kura,huku pia Mkurugenzi wa technologia ya habari na mawasiliano TEHAMA wa tume ya uchaguzi DK SISTI CARIAH akiondolewa kwenye nafasi hiyo kukiwa kumesalia mwezi mmoja kupiga kura.

Mabadiliko mengine ambayo TACEO wameonyesha kuwa na wasiwasi ni kuteuliwa kwa makamishna wawili wa tume hiyo zikiwa zimebaki siku 39 kabla ya siku ya kupiga kura ambapo walioteuliwa kushika nafasi hiyo ni pamoja na Jaji mstaafu wa mahakama kuu ya Tanzania,MARY LONGWAY na wakili ASINA A,OMARY

Wakili IMELDA amesema kuwa mtandao huo unaitaka serikali kuhakikisha kuwa hawafanyi mabadiliko ya tume ya uchaguzi kwa kuwaondoa watendaji wake kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha mapungufu ya kiutendaji ndani ya tume na kupelekea wananchi kukosa imani na tume hiyo.

Aidha katika hatua nyingine mtandao huo wa TACCEO umeitaka tume ya taifa ya uchaguzi NEC kuhakikisha kuwa inatangaza na kuweka wazi orodha ya vituo vya kupigia kura mapema ikiwa ni pamoja na kuweka daftari la wapiga kura siku 14 kabla ya uchaguzi ili wananchi waweze kuhakiki majina yao na kufahamu vituo wanavyostahili kutumia kupiga kura.

Mtandao wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO unaoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC umekuwa ukishiriki katika uangalizi wa mchakato wa uchaguzi nchini kuanzia zoezi la uandikishwaji wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektonic BVR, mchakato wa kuwapata wagombea ndani ya vyama,kampeni za Urais,wabunge na madiwani kuelekea mchakati mzima wa uchaguzi wa tarehe 25 october mwaka 2015.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top