Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi
wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma
(hawapo pichani),alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya
kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni.
PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.
PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru kiongozi huyo wa dini
kwa kujitolea kumuombea Dua ya heri na afya njema katika nafasi yake ya
kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia
wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani
Ikungi mkoani Singida jioni ya leo ,wakati akiwaomba wananchi hao kumpigia kura za
ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na
Madiwani.
Dkt. Magufuli amesema serikali
yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali hasa za mashirika ya
dini ambazo zinaendesha hospitali katika kupata vifaa, Ruzuku, na
ajira kwa wafanyakazi ili kuimarisha huduma za kiafya kwa jamii.
Sehemu ya umati wa Wakazi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi kwenye mkutano wake wa mwisho kwa jioni ya leo,ambapo kesho anatarajia kuendelea na kampeni mkoani Singida na baadae kuhitimisha kampeni zake kwenye mkutano mkubwa ambao unatarajiwa kurushwa live na kituo cha Star TV.
Kiongozi
wa Msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli,Ndugu
Abdallah Bulembo akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt.Magufuli
kuwahutubia wananchi wa Ikungi jioni ya leo na kuwaomba kumpigia kura ya
ndio ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchahuzi mkuu wa Urais,Wabunge
na Madiwani.
Wananchi
wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika
katika uwanja wa
Mnadani Ikungi mkoani Singida,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John
Pombe Magufuli aliwahutubia na pia kuwaomba wananchi hao kumpigia
kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais ,
Wabunge na Madiwani.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia
debe Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk.
John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika
uwanja wa Mnadani Ikungi,mkoani Singida.
Msafara
wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili mjini Itigi mkoani
Singida mapema leo mchana,tayari kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni
mjini humo.
Baadhi
ya Wazee wakifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya wananchi wa mji wa Itigi mkoani
Singida mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Baadhi
ya Wakazi wa mji wa Manyoni wakishangilia jambo kwenye mkutano wa
kampeni wa hadhara wa Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na
kuwaomba kura ili awe Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,ambapo ameaomba ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeze kwa
wingi kumpigia Kura za Urais,Ubunge na Udiwani..
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi
(CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la
Manyoni Mashariki Ndugu Damiel Mtuka mara baada ya kukabidhiwa Kitabu
cha Ilani ya chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
uliofanyika mapema leo mchana mjini Manyoni mkoani Singida
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Manyoni wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la
Itigi Ndugu Yahaya Omar Masele mbele ya Wakazi wa mji huo (hawapo
pichani),waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika
mapema leo mchana.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge
jimbo la Itigi Ndugu Yahaya Omar Masele mbele ya Wakazi wa mji huo
(hawapo pichani),waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
uliofanyika mapema leo mchana.
Baadhi
ya wananchi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa
kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa
akijinadi.
Post a Comment