Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mara
Mheshimiwa Capt. Mstaafu Aseri Msangi mara baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Musoma kwa ziara ya siku mbili mkoani humo tarehe
2.10.2015. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara.
Mama
Salma Kikwete akifurahia ngoma ya utamaduni na wananchi wa Kijiji cha
Nyamwaga kilichoko katika wilaya yaTarime kwa ajili ya kuzindua rasmi
Shule ya Sekondari ya J. K. Nyerere iliyojengwa na Kampuni ya Acacia
inayomiliki Mgodi wa North Mara Gold Mine
Mama
Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya utamaduni na wananchi wa
Kijiji cha Nyamwaga kilichoko katika wilaya yaTarime kwa ajili ya
kuzindua rasmi Shule ya Sekondari ya J. K. Nyerere iliyojengwa na
Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa North Mara Gold Mine
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiteta
jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu Glorius Luoga muda mfupi baada
ya kuwasili kwenye Kijiji cha Nyamwaga kwa ajili ya uzinduzi wa Shule ya
Sekondari J K Nyerere.
Mama
Salma Kikwete akijumuika na viongozi wa Mkoa wa Mara na wanachi wa
Kijiji cha Myamwaga kusherehekea uzinduzi rasmi wa Shule ya J.K. Nyerere
iliyojengwa na North Mara Gold Mine.
Mama
Salma Kikwete akitoa hotua ya uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari
J.K.Nyerere katika Kijiji cha Myamwaga kilichoko Mkoani Mara.
Mama
Salma Kikwete akishirikiana na viongozi wa Mkoa wa Mara na wale wa
Wilaya ya Tarime na wahisani waliojenga Shule ya J.K. Nyerere kukata
utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Shule hiyo iliyoko katika
Kijiji cha Nyamwaga.
Mama Salma Kikwete baada ya kukata utepe hapa anakiondoa kitambaa kukamilisha sherehe ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza Ndugu Jimmy Ijumba, Meneja wa
ACACIA –North Mara Gold Mine mara baada ya kuzindua rasmi shule hiyo
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga
ikiwa ni ishara ya kuagana nao baada ya kuifungua rasmi Shule ya
Sekondari J.K. Nyerere iliyoko katka Wilaya ya Tarime.
Mama
Salma Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali wakati akiingia eneo
la Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwenye uzinduzi wa uboreshaji wa
miundombinu katika hospitali hiyo.
Mama
Salma Kikwete akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Capt. Mstaafu
Aseri Msangi na Ndugu Glorius Luoga, Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuondoa
kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa uboreshaji wa hospitali hiyo.
Baada
ya kuzindua rasmi uboreshaji wa hospitali ya Wilaya ya Tarime, Mke wa
Rais, Mama Salma Kikwete anapanda mti wa kumbukumbu kwenye eneo la
hospitali hiyo.
Mama Salma Kikwete akipiga picha na wanachuo wanaosomea uuguzi katika Hospitali ya Wilaya Tarime.
Akina
mama waliojitokeza kuja kuongea na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
wakicheza kwa furaha mara baada ya Mama Salma kuingia ukumbuni.
Mwenyekiti wa WAMA,Mama Salma Kikwete akiwapungia kwa furaha akinamama wa Tarime muda mfupi kabla ya kuongea nao tarehe
Mwenyekiti wa WAMA,Mama Salma Kikwete akiongea akinamama wa Tarime. Picha zote na John Lukuwi
Post a Comment