Mgombea
ubunge jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule. (Na
Mpigapicha Wetu)
Mgombea
ubunge jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha akimnadi mgombea ubunge
jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu (kushoto) wakati wa
uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha akimnadi mgombea ubunge
jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu (kushoto) wakati wa
uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule.
Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za mgombea wa ubunge wa Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu.
Mgombea wa Ubunge katika jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu (kushoto) akitambulisha wagombea wa udiwani wa kata za jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, kwenye uzinduzi wa mikutano ya kampeni zake.
Wanachama wa CCM wakiwa katika mkutano huo.
Mgombea Udiwani Kata ya Mbagala Kuu, Yusuf Manji akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa ubunge wa jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu kwenye uzinduzi wa mikutano ya kampeni zake.
Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA wa Ubunge wa tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) jimbo jipya la Mbagala Issa Mangungu, amesema
endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha vijana
wanapewa kipaumbele katika kupata ajira.
Mangungu aliyasema hayo juzi wakati wa uzinduzi rasm wa kampeni zake katika jimbo hilo, zilizofanyika kwenye viwanja vya
Chamazi Shule Jijini Dar es Salaam, kuwa atahakikisha suala la ufundi kwa vijana linapewa kipaumbele.
Alisema
katika kuhakikisha vijana wanapata ajira ataishawishi Serikali kufungua
tawi la Chuo cha Ufundi (VETA), katika Jimbo hilo ili vijana waweze
kusoma na kupata
kazi.
"Nitahakikisha napigania uanzishwaji wa tawi la Veta katika la Mbagala
hili vijana waweze kupata mafunzo ya ajira"alisema Mangungu. Katika
hatua nyingine Mangungu alisema kuna tatizo la shule katika baadhi ya
kata atahakikisha wanajenga shule ili kuepusha wanafunzi kutembea kwa
muda mrefu kupata elimu.
Alisema
kuna tatizo la kutokuwa na Shule za Sekondari haswa za kuanzia kidato
cha tano, hivyo watajipanga kuongeza madarasa na kujenda shule nyingine
za Sekondari."Kwenye sehemu ya shule za Sekondari tutaongeza majengo ya
madarasa ili wanafunzi wakaofanya vizuri wapate nafasi ya kuendelea na
kuna kata nyingine tutajenga shule za Sekondari"alisema Mangungu.
Alisema
kuwa katika upande mwingine atahakikisha madereva wa bodaboda
wanatambulika kwa sababu nao ni wapo kwenye ajira.Mangungu alisema kuwa
lazima madereva wa bodaboda wawe kwenye ajira rasmi, hivyo kama mbunge
atawatetea madereva hao.
Alisema
kuna tatizo la Maji na Barabara vipi ndani ya vipaumbele vyake ana
amini akipata nafasi yeye na madiwani wake wa CCM watafavifanyia kazi.
Mangungu amewataka wakazi wa mbagala kumchagua yeye katika nafasi ya ubunge, ikiwa pamoja na kumchagua mgombea wa Urais
John Magufuli na kuchagua madiwani wa CCM, ili waweze kuwa kitu kimoja na kuweza kushirikiana katika kuwaletea maendeo.
Katika
mkutano huo wa ufunguzi wa Kampeni ya za mbunge huyo, mgeni rasmi
alikuwa Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa (NEC),
ambaye aliwataka wakazi wa jimbo hilo wasifanye makosa kumchagua mbunge
wa upinzani.
Nahodha alisema ana amini wakimchagua mbunge, Rais na madiwani wa CCM wataweza kufanikisha ahadi zao.
Alisema CCM ina ilani nzuri inayotekelezeka kwa wananchi wake hivyo kuna kila sababu ya kulitambua hilo.
Naye
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, amewataka
wananchi wa jimbo hilo kutofanya makosa ya kuwapata uongozi wa wa vyama
vya upinzani, kwa sababu hawana sera, hivyo watumie nafasi hiyo kuchagua
wagombea wa CCM.
Madabida
alisema kuwa siku ya Oktoba 25, wahakikishe wanajitokeza kwa wingi
kwenda kuwapiga kura na kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Katika
mkutano huo mgombea Ubunge aliwatambulisha wagombea Udiwani wake katika
Kata 10 zilizopo katika Jimbo hilo akiwemo Yusuph Manji na Said Fella.
Post a Comment