THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewateua wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi wengine
saba.
Wakuu
wa wilaya 13 walioteuliwa ni Shaaban Athuman Ntanambe ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara; Richard Kasesera ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth Msafiri ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma na Abdallah Njwayo
ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Wakuu
wa Wilaya wengine wapya ni Asumpta Mshama ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye anakuwa
Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe; Honorata Chitanda ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga na Christopher
Ng’ubyagai ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida.
Wakuu
wengine wapya ni Hawa Ng’humbi ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kishapu, Mkoa wa Shinyanga na Mrisho Gambo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma.
Wakuu
wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka
Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha;
Wilson E Nkambaku ambaye anahamishiwa Arumeru, Mkoa wa Arusha kutoka
Kishapu, Mkoa wa Shinyanga; Francis Miti ambaye anahama Wilaya ya
Hanang, Mkoa wa Manyara kwenda Monduli, Mkoa wa Arusha na Jowika Kasunga
ambaye anahamia Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa kutoka Monduli.
Wengine
waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Wilaya ya Makete, Mkoa wa
Njombe kwenda Wilaya ya Morogoro; Hadija Nyembo ambaye anahamia Wilaya
ya Kaliua, Mkoa wa Tabora kutoka Uvinza, Mkoa wa Kigoma na Benson
Mpyesya ambaye anahamia Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma kutoka Kahama.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
04 Oktoba, 2015
Post a Comment