Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mkurugenzi mkuu wa TANESCO aongea kuhusu mgao wa Umeme

 Mkurugenzi wa TANESCO Injinia Felichesmi Mramba ametaja sababu za kukata kata umeme hapa nchini kama ifuatavyo:- 
  1. Dar es salaam katikati ya jiji kuna mradi wa umeme unaojengwa kwa kushirikiana na serikali ya Finland ya kujenga kituo kipya cha umeme katikati ya jiji kitakachokamilika Novemba 2015 hivyo maeneo ya Ilala, Makumbusho na katikati ya jiji yamekua yakizimiwa umeme sababu ya kazi inayoendelea.
  2. Arusha kuna kituo kikubwa cha Njiro kimejengwa upya ambapo mjenzi amemaliza kazi yake ila kinachoendelea ni kuunganisha kituo kipya na laini zinazosambaza umeme Arusha.
  3. TANESCO imeanza kuwasha mitambo baada ya gesi kufika Dar es salaam hatua kwa hatua kadri presha inavyofika kwenye bomba, mtambo wa kwanza uliwashwa September 17, mitambo imekua ikiendelea kufanyiwa kazi na kuwasha hadi leo.
  4. Ikifika tarehe 9 au 10 October 2015 tatizo la kukatika kwa umeme linaweza kuwa limepungua kwa kiasi kikubwa ila tarehe 20 October tatizo ndio litakua limemalizika kabisa nchi nzima.
  5. Kilichoandikwa kwenye gazeti kwamba TANESCO haina pesa ndio maana hakuna umeme ni UONGO.
  6. Wananchi wawe na subira, bomba la gesi lilikua jipya na uwashaji mitambo hauwezi kufanywa yote kwa mara moja au kwa siku moja, ni lazima uende taratibu lasivyo kazi tuliyoifanya kwa miaka miwili tunaweza kuiteketeza ndani ya wiki moja.
  7. Mitambo mingine ikiendelea kuwashwa hivi karibuni Dar es salaam haitaathiriwa tena na kukatika kwa umeme ila mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya itapata mkato kidogo mpaka tarehe 7 October, baada ya tarehe 7 Wananchi wataona mabadiliko wenyewe.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top