Tume
ya taifa ya uchaguzi imesema haitaruhusu mawakala wa vyama vya
NCCR-Mageuzi, CUF na NLD kuingia katika nyumba vya kuhesabia kura za
wagombea urais kwa kuwa havina mgombea wa nafasi katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa mkutano ya viongozi wawakilishi wa
wanawake, mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Bwana Kailima Kombey, amesema
tume ya taifa ya uchaguzi haitambui umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA-
bali inamtambua kisheria mgombea urais kwa tiketi ya chama cha demokrasi
na maendeleo-Chadema- chama ambacho kinapaswa kuteua mawakala wa
kuwasimamia wagombea.
Kuhusu
hofu ya uwazi katika upigaji na kuhesabu kura, mwenyekiti wa tume ya
taifa ya uchaguzi, jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kura zote
zitapigwa na kuhesabiwa katika vituo chini ya usimamizi wa mawakala wa
vyama na waandishi wa habari wataruhusiwa kuingia, na kusisitiza vyama
vya siasa vinavyoshawishi wapigakura wao kubaki katika vituo kulinda
kura vinaajenga ya kusababisha usumbufu na uwoga kwa baadhi ya wananchi
utakaosababisha kutojitokeza kupiga kura.
Mwakilishi
wa mtandao wa asasi za kirai mkoani Tanga Bi.Adela Mtei ameilalamikia
tume ya taifa ya uchaguzi kwa kukaa kimya huku baadhi ya viongozi wa
vyama vya siasa wakitoleana na matusi na kashfa badala kutangaza sera
hali inayotoa hofu kwa wanawake kuweza kujitokeza Oktoba 25 kutimiza
haki yao ya kisheria ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Post a Comment