BAADA
ya kutokea kifo cha Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila
maeneo ya Msolwa, Chalinze, mkoa wa Pwani, kuliibuka hisia nyingi
kutokana na chanzo cha kifo hicho, ifuatayo ni taarofa ya jeshi la
Polisi mkoa wa Pwani:-
Mnamo
tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu
barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze,
Mkoa wa Pwani. Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na
George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam
liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher
Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na
mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni “B” Dar Salaam.
Katika
ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu
Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa
Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani,
mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji wa Kanisa la
Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na
michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka
31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la
mabegani. Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya
Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na
waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.
Baada
ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa
ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa
Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe,
Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha
wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A.
Makata.
Uchunguzi
wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari
aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana
tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na
kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu
kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.
Kabla
ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni
waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe
03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa
huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na
kusababisha uharibifu wa gari lao.
Kulingana
na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe
walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.
Tarehe
03/10/2015 saa 21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na
ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.
Uchunguzi
uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika
eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo
la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa
na sababu zifuatazo:
- Mwendo kasi, dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa. Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.
- Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
- Kutofunga mkanda ya usalama. Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).
- Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.
Hivyo
nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda
mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha
niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale
watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia
hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim.
Post a Comment