Na Mwene Saidi wa Globu ya Jamii
Rufaa
iliyokatwa na mawaziri wa zamani Basil Mramba (kushoto) na Daniel
Yonah imegonga mwamba katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es
Salaam leo, baada ya kuwapunguzia mwaka mmoja na kuwaondolea faini ya
milioni 5 na kutakiwa kuendelea kutumikia kifungo cha miaka miwili
baada ya mahakama hiyo kuona hakuna ushahidi wa kuthibitisha shitaka la
kusababisha hasara ya Sh. bilioni 11.7.
Kadhalika,
mahakama hiyo imesema Mahakama ya Kisutu, ilikuwa sahihi kumwachia huru
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja kwa kuwa hakuna ushahidi
uliothibitisha kuhusika na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na
kusababisha hasara hiyo.
Hukumu
hiyo iliyosomwa kwa saa mbili saa 3:28 hadi 5:00 na Jaji Projest
Rugazia aliyesikiliza rufaa mbili zilizokatwa na pande zote mbili dhidi
ya kesi hiyo.
Awali
upande wa Jamhuri ulikata rufaa kupinga hukumu ya kumwachia huru Mgonja
na utetezi ulikata rufaa kupinga hukumu ya kuwatia hatiani Mramba na
Mgonja.Jaji Rugazia alisema hakuna ushahidi ulitolewa mahakamani kueleza
namna gani washtakiwa walihusika kusababisha hasara na kwamba adhabu ya
kosa hilo ilitolewa kimakosa dhidi ya washtakiwa.
Alisema kulingana na ushahidi uliotolewa hakuna lawama kwa Mahakama ya
Kisutu, kumwachia huru Mgonja dhidi ya mashitaka yaliyokuwa yanamkabili
kwenye kesi hiyo.Pia, alisema haoni kama kuna sababu ya kumhusisha rais
(wakati huo Benjamini Mkapa) kwa kuwa alitoa maelekezo kulingana na
maelezo aliyopewa na mshtakiwa wa Yona.
"Sioni
sababu ya kumtumia rais kwa makosa yaliyotokea kwa kuwa alitoa maekezo
kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na mshtakiwa wa pili, Yona... pia
hakuna ushahidi uliowaweza kuelezea mahakama namna gani washtakiwa
walifanya kosa la 11 la kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni
11.7, mahakama hii inatengua adhabu ya kosa hilo na washtakiwa
watatumikia kifungo cha miaka miwili kila mmoja" alisema Jaji Rugazia.
Mapema
Julai 6, mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es
Salaam, iliwatia hatiani washtakiwa hao na kumwachia huru Mgonja.
Wafungwa hao kwa pamoja wamekutwa na hatia ya makosa 10 ya kutoa
msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government
Business Corporation kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa madini ya dhahabu
nchini.
Post a Comment