WAZALENDO – 2015
1)
AWAMU YA TANO NDO
HII, VIONGOZI KAMPENINI
TWAMUHITAJI
SAHIHI, WALA SIO WA UTANI
HAPA HAKUNA
KUWAHI, SAFARI HII TUKO MAKINI
2)
SAFARI HII
TUMECHOKA TWAWATOLEENI UVIVU
SISI
TUNAWAAMINI, NDO MAANA TWAWAPA SHAVU
KURA
TUKIWAPIGIA, ILI MUWE WASIKIVU
KISHA MNATUGEUKA,
KUTUONA WAPUNGAVU.
3)
USO KWA USO TU
LIVE NA IMANI ZENU POTOVU
KWA NINI
MWANG’ANG’ANIA, MPAKA MUWE VIONGOZI
HAPO HAPO
KUNA SIRI, NDO MAANA MWAOTA SHAVU
SISI
TUNADHOOFIKA, NYIE MWAZIDI KUNONA.
4)
IMEKUWA SIKU
NYINGI, WAZALENDO TWATESEKA
WALO FAIDI
KWACHACHE WENGI TUMESAHAULIKA
RUSHWA KOTE
IMETAWALA, MASIKINI HANA HAKI
NJOO UTOE
UCHAFU, TANZANIA IACHE NUKA.
5)
NYIE WATU
MMEROGWA, MWAHITAJI KUOMBEWA
DUNIANI KUWA
BINGWA, MKASAHAU AKHERA
HAMUOGOPI
ULINZWA, NCHI MLIONGOZAJE
TAMAA
MWAWEKA MBELE, UMAUTI WENU NYUMA.
6)
SASA UMEKUWA
MCHEZO, UONGOZI KUGOMBEA
PESA
MNATUMWAGIA, KISHA MNATUNYAKUA
MIDOMO
MMETUGUNGA, HATUWEZI FURUKUTA
MWALIMU
ALITUONYA, MKWEPWE KAMA UKOMA.
7)
MWAMWAGA PESA
HADHARANI, BILA HATA YA KIFICHO
HAYA
ZIMWEKURUKENI, KANA KWAMBA HATUNA MACHO
HII SASA SI
SAISA, NI YA MWENYE KUWA NACHO
KWA MIPANGO
YA MANANI, ATAPITA ALOMPANGA.
8)
HATUHITAJI MAPESA
KILIO CHETU USAWA
ATACHO PEWA
MENEJA NA MKULIMA IWE SAWA
SIO MWENYE
KUTUUMA-NA KUPULIZA KAMA PANYA
KUTUACHA NA
BUTWAA – JINSI ATAKANYOTUNYONYA.
9)
TWAWAONYA
WAZALENDO, WENYE AKILI TIMAMU
TUACHENI
KUPUMBAZWA – NA WAUCHU WA UONGOZI
ANATUPIA
TUKANGAA – NA AHADI ZA UONGO
MGOMBEA WA
KUHONGA – AKIFIKA IKULU NI SUMU.
10)
TUMKUNJENI
SAMIKI, BADO ANGALI MBICHI
WALE WEZI WA
ZAMANI, SISI HATUWA SADIKI
FISADI HUWA
HASIKII, NA WIZI WAKE AACHI
MWIZI SISI
HATUMTAKI, WACHA TUMEACHE BENCHI.
11)
JAMANI SISI TUMECHOKA,
MWENYEZI MUNGU SHAHIDI
KIONGOZI
TUNAETAKA JULETUTAE FAIDI
WATUFANYA
BURICHEKA, KWAMUOGOPI WADUDI
WAJIONA
WAMEFIKA, HWA MOLA HAWATORUDI.
12)
KWA MANANI
TUMEOMBA TUNASUBIRI NUSURA
YEYE PEKEE
NDO MUUMBA AATAELETA NUSURA
NA HAWA NDO
KAWAUMBA INGAWA SI WATUKERA
TUNAKUOMBA
RABUKA, TUKINGE NA SHARI ZAO.
12A)
MZALENDO SI MGENI NJOO MWENYEJI AHAME
WAMEBAKIRI
KAULI, NJOO MWENYEJI AHAME
KUMUHIMISHA
MWENYEJI, UKAMFADHIRI MGENI
JAMANI HII
NI DHURUMA, ISO KUWA NA MFANO.
13)
SIO WOTE
NI WACHAFU WAPO WENGINE WASAFI
WAO
NI WAADILIFU, HAWA SIO MABEPARI
HAWANA
HATA KASIKENDO WANA SIKIKA KWA WEMA
KURA
ZETU TUWAPE LEO, KESHO NASI TUFURAHI.
14)
TWAHITAJI
MWANDIRIFU, MWENYE MOYO WA IMANI
ATAE ONDOSHA
MACHAFU, NA KUENDELEZA MEMA
KWA MOLA AWE
NA HOFU, AJUWE WAJIU WAKE
MWENYE ROHO
SIO CHAFU, NA KUWAJALI WENZAKE.
15)
TWAHITAJI
MWANADAMU, HAIJARISHI CHAMA GANI
AMBAE HANA
HASIRA, KUTUTIA UTATANI
WALA SI KING’ANG’ANIZI,
ASO KUBARI KUSHINDWA
ASIYE TAKA
MAKUU, AJIWEKA KAWAIDA.
16)
HAIJARISHI DINI
GANI, ILI MRADI ANA IMANI
IKIWA NI
MCHA MUNGU, SISI TUTAPATA AMANI
SI MBAGUZI
WA DINI, KABILA AU HALI GANI
ATAEJALI-MAENDELEO
YA WANACHI NCHINI.
17)
TUNASISITIZA
UUTU- KWA HUYU MPYA KIONGOZI
ATAMBUE NASI
WATU, ASUTIE SIMANZI
AJUE HAPA NI
KWETU, SI TU KWA AKINA FULANI
WAZALENDO TU
NYUMBANI, HAPA SIO UGENINI.
18)
KUMBUKA ALOKUPA
CHEO, NI MWENYEWE MTUKUKA
TUFANYIE
UWADIRIFU, ASIJE KUKASIRIKA
USIJE KUWA
KINYONGA, NA KUGEUKA KUWA NYOKA
KAMWE
HATUTOKUWEZA SHAHIDI ATAKUBUKIKA.
19)
TWASHITAKI KWA
MUUMBA, RAIS WETU SHAHIDI
VITUKO VYA
MAFISADI, TANZANIA VIMEZIDI
WAMEGEIZA
SIASA, KITENGO CHA UFISADI
UKIINGIA
IKULU – WEKA MAGUFURI WASIRUDI.
19A) HII
DEMOKRASIA – SI NCHI YA KISURUTANI
AWAMU HII YA
TANO SIO YA KURISHANA
TUSHAMUONA
MSAFI SISI TOKEA ZAMANI
YEYE NDO CHAGUO LETU WALA HANA MPINZANI.
19B) MWENYE
AKILI AFIKIRIE TUSICHEZEE BAHATI
ALOTUPAPELI
AWAKI-ATUTOBOA JICHO KWA KIJITI
MWIZI HATA
ASUGULIWE KWA JIKI WALA HATAKATI
NAMCHAGUA MSAFI,
FISADI KULA YANGU HAPATI.
20)
ONA HAWA MAFISADI
KUTUFANYA PUNGUWANI
TANGU LINI
MTU UIBE NA UFUKUZWE KAZINI
WEWE WEWE
TENA URUDI, ETI USHIKE USUKANI
HIKI JAMANI
NI KIOJA CHA KARNE DUNIYANI.
21)
MAFISADI MIAKA
YOTE HULA WAO PEKE YAO
SAFARI HII
WATUZUGA ETI NASI TULE NAO
HII NI
DANGANYA TOTO, TUMEJUA MBINU ZAO
TUNAMTAKA
MSAFI, ALOMESH HILA ZAO.
22)
KUNA TOFAUTI
KUBWA TAJIRI NA MASIKINI
ZAMANI WASHAPUUZWA
HAWAJUI WALA NINI
FISADI NA
MATAJIRI KULA YAO MOJA SAHANI
HAWAHITAJI
RAIYA WAO HUTEMBEA ANGANI.
23)
WAMESHUKA ONBA
KURA TENA KWA KUHONGA PESA
UTAJIRI
WAKINADI ETI NI WANA SIASA
HALI HII
WALIPITA CHA MOTO TUTAKIONA
MOLA ATUPISHE
MBALI IKULU WASIINUSE.
24)
RAIS ASIINGILIWE
KATIKA MAAMUZI YAKE
TARATIBU
AZIPANGE KUTIMIZA AHADI ZAKE
AKIHITAJI
USHAURI BILA SHAKA ATAKWETENI
ILA
MSIMVURUGE NA ROHO ZENU ZA KWANINI.
25)
UKISIKIA RAIYA,
AHITAJI MSAADA
HARAKA
MTUMIZIE, UONDOE YAKE SHIDA
MA WEWE
IKIMPUUZA ATAKOSA HATA PAWENDA
JOHN JALI
MZALENDO NA SISI TUTAKUPENDA.
26)
USIFANYE
TUJUPENDE MPENDEZE MOLA WAKO
ALO KUPA
HICHO CHEO, NA HIZO PUMZI ZAKO
UONGOZI
ALISHA TAJA, NASI TUWE NYUMA YAKO
SASA
TUFANYIE WEMA, ASIJE KUCHAPA VIBOKO.
27)
PENDELEA MASIKINI
UFUKARA HAKUUOMBA
FISADI
ALIMUWAHI PESA ZOTE AKAKOMBA
TANZANIA
ITAJIRI HAIITAJI OMBA OMBA
RAIS KILA LA
KHERI NYUMA SI TWASHIRI KAMBA.
28)
RAIS UJITOLEE
KUWEKEZA VIJIJINI
HUKO
WAMEWAPUUZA KANA KWAMBA SI NCHINI
MASIKINI
WANYAMAZA NA HAWAJUI KUNA NINI
UKIMYA WAO
SI BURE ISIJE KUWA WA LAANI.
29)
BARA PIA VISWANI
– NI MUUNGANO WA NCHI MOJA
WAZALENDO
HAPA NCHINI, SISI NI KITU KIMOJA
BARA TWATAKA
RIDHIKA, PEMBA MPAKA UNGUJA
RAIS WA
MUUNGANO NDO HUYO TUNAMMGOJA.
30)
THEHEBU KUBWA NI
MBILI WAKRISTO NA WAISLAM
WOTE
TUHESHIMUMIANE NA KUPEANA SALAAM
NJE
WANATUTAMANI, TUNAVYOISHI KWA SALAMA
MFANO WA
JIJI LETU, BANDARI YA SALAMA.
31)
ELIMU KWETU
MUHIMU MAVAZI PIA MAKAZI
TUTIBIWE
KIRAHISI TUYAPATAPO MARADHI
AJIRA ZIWE
KWA WINGI, NASI TUSHIRIKI KAZI
USALAMA
UBORESHWE KUKOMESHA MAJMBAZI.
32)
MSAFI TUMAKUOMBA
ZIDISHA ZAKO JUHUDI
TANZANIA
ISAFISHE UUTUTE UFISADI
MAFISADI
WASHATOKA, UZUIE WASIRUDI
SIFA YETU YA
ANAMI, TUUMBE MUNGU IRUDI.
33)
MACHAFUKO
TUYAKWEPE, KWANI VITA HAINA MACHO
MIFANO
TUNAIONA, KWANI HAINA KIFICHO
WENZETU
WANAUWANA HAWANA PA KUJIFICHA
IKIANZA
IMEANZA, KAMWE HAIWEZI ACHA.
34)
TWAWAONYA
MAJIRANI WASIO JALI AMANI
KWAMBA TOKEA
ZAMANI, TUMEITUNZA AMANI
TUNACHOLINDA
AMANI, BARA MPAKA VISIWANI
TANZANIA YA
AMANI, JADI YETU NI IMANI.
35)
TUNAINUA MIKONO
MOLA ASISHUSHE GHARIKA
UONEVU
UKIZIDI – WOTE SI TUTADHURIKA
YEYE PEKEE
NDO ANA SIRI HUKUMU YAKE IKIFIKA
TUSHIKANE
KWA MAOMBI MUNGU ATATUITIKA.
36)
TUNAINUA MIKONO
KUOMBA KWAKO RABUKA
HATUNA SI
KIMBILIO, ILA KWALO MTUKUKA
RABBI ONDOA
VILIO, WAZELENDO TWATESEKA
TUTUNUKU
KIONGOZI NA SISI TUPUMZIKE.
37)
TUMIMINIE BARAKA
ISAMBAE DUNIANI
ISITOKEE
GHARIKA , KUJA KUTUANGAMIZA
TUACHE KUTENDA DHAMBI, TUMUOGOPE MANANI
TUWE WATU WA
UPENDO UTUKINGE NA SHETWANI.
38)
NIMEZALIWA
TANZANIA NIMEKULIA TANZANIA
MIMI
NAJIVUNIA KUITWA MTANZANIA
NAPIGANIA
NCHI YANGU, SWEET HOME TANZANIA
MOLA
TUSHUSHIE NEEMA – TANZANIA YA WATANZANIA.
UTENZI HUU
WA WAZALENDO NI ZAWADI KWA RAIS WETU MSAFI,
MPENDWA,
MTARAJIWA. EWE MOLA WETU TUALALIE UCHAGUZI 25/10/2015 UWE WA SALAMA NA AMANI.
Post a Comment