Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama
Salma Kikwete akiwapungia mkono viongozi na wanachama wa UWT wa Mkoa wa
Mara wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre kwa ajili
ya mkutano wa ndani na wanachama hao-Octoba 3, 2015.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachama wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT) wa Mkoa wa Mara wakati alipokutana nao kwenye
ukumbi wa Musoma Community Centre.
Umati
wa wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Mara wakimsikiliza kwa
makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati alipokuwa
akiongea nao Mjini Musoma.PICHA NA JOHN LUKUWI.
Na Anna Nkinda – Tarime.
Wanawake wilayani Tarime wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura
siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu itakapofika
na wachague viongozi watakaowaona wanafaa ambao watawaletea maendeleo.
Rai hiyo imetolewa leo na Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanawake wa wilaya hiyo
iliyopo mkoani Mara katika ukumbi wa mikutano uliopo katika hoteli ya
CMG.
Mama
Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM
kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema kupiga kura ni haki ya kila mtu
hivyo basi haitakuwa busara kwa wanawake
hao kuharibu kura zao kwa kukaa majumbani siku ya uchaguzi ikifika bali
waende kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha .
“Kura
ni siri ya mtu, wewe ndiye unayefahamu kiongozi gani wa kumchagua
nawasihi chagueni viongozi wazuri na siyo bora viongozi, wahimizeni
wanawake wote waliojiandikisha washiriki kupiga kura kwani kura zenu
yako ndiyo itakayokupatia kiongozi unayemtaka”, alisema Mama Kikwete.
Alisema
siasa siyo uadui wala ugomvi bali ni mchakato wa kidemokrasia na
kuwataka wagombea wote kunadi sera zao kwa kufuata utaratibu na amani
kwa kuzingatia kanuni na sheria zilizopangwa na tume ya Taifa ya
Uchaguzi ili utulivu na Amani viendelee kutawala nchini.
Aliwasihi,
“Msigombane kutokana na tofauti ya itikadi za vyama vya siasa,
angalieni siasa zisiwafarakanishe ikafika hatua mkashindwa hata
kusaidiana ikiwa ni pamoja na kushindwa kuzikana kumbukeni nyinyi ni
ndugu wa wilaya moja ya Tarime”.
Aidha Mama Kikwete aliwataka wanawake hao kujenga tabia ya kujiwekea
akiba Benki kutokana na fedha wanazozipata katika kazi wanazozifanya
kwa kufanya hivyo wataweza kukopa fedha nyingi ambazo watafanyia
shughuli za maendeleo na hivyo kujikomboa kiuchumi.
“Unganeni pamoja
ili muweze kujikwamua kiuchumi, simameni katika majukwaa teteeni haki
zenu, pingeni mila zilizopitwa na wakati ambazo zinamkandamiza mwanamke
na hivyo kumrudisha nyuma kimaendeleo kwa kufanya hivyo mtaweza
kujikomboa kutoka katika hali ya unyanyasaji”,alisisitiza .
Post a Comment